ACT -Wazalendo kwa Mpina walikumbatia mzinga wa nyuki wakidhani ni gogo la mbao ngumu.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
18,154
Reaction score
17,491
Sijui ni kwanini wapinzani hawakomi, kila uchaguzi wananaswa kwa mtego uleule wa CCM unaotegwa kwa aina ileile na kunaswa palepale chini ya mkanda. Orodha ya mitego ni ndefu sana (Marando, Mrema, Prof. Lipumba, Dr. Slaa, Lowassa, Sumaye, Lamwai, Mpina, Membe).

Iko hiviii!! Kule CCM huwezi kufikia ngazi ya kukabidhiwa uwaziri kama wewe sio CCM hasahasa na mwenye sifa za ziada za uzalendo kwelikweli. Ila kila uchaguzi unapokaribia wanatengeneza mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe (mtego) ambao utaiva wakati wa kuteuana nani awe mbunge na nani awe Rais kupitia CCM. Ikifikia hapo mtu huyo maarufu na machachari mwenye hadhi angalau ya ubunge/uwaziri/uwaziri Mkuu atasukumizwa nje ya chama au atakatwa na kujifanya ana hasira kali sana kwa kukatwa visivyo halali au kusukumizwa nje ya chama. Masikini vyama vya upinzani kwa wengine kujua na wengine kutokujua watamnyakua harakaharaka kiongozi huyo maarufu kuja kuwa mgombea wao wa Urais. Na hapo ndiyo safari yao ya kuukumbatia mzinga wa nyuki itakapoanzia wakichani wamepata gogo la mninga kubwa wachane mbao wapaulie nyumba yao mbovu.

Wagombea hawa kutoka CCM mara zote ni chambo kwa vyama vya upinzani, wanajua wanakwenda kufanya nini kule, na wakishamaliza watarudi nyumbani CCM kupunzika na kuendelea kula mema.

Wapinzani walinaswa na mtego huu kwa miaka mingi sana lakini hawashituki. Hawashituki kwasababu ama na vyama vya upinzani yamo mapandikizi pia au wapinzani ni dhaifu sana hata wa kufikiri tu au wanajua ila lengo lao ni kupata wabunge na ruzuku tu kwa ongezeko la kura watakazopata kupitia mheshiwa yule.
 
Kwambthadi sasa NRNE haina maana yoyote kwao kama si midoli basi ni wazimu wa kiwango cha lami!
 
Hakuna viasharia vyovyote kwamba huyo ngosha ni mpinzani kazi maalum!
 
Kakaa ili uteuliwe kuwa waziri miongoni mwa wanaCCM wengi lazima uwe mtu na nusu. Mgogoro wa Mpina ndani ya CCM ni wakutengeneza, na matumizi yake yalikuwa muda huu na amemaliza kazi aliyotumwa kwa dakika moja tu. Sababu za kuenguliwa zizo wazi hata mwehu inaziona bila kumulikiwa.
 
Back
Top Bottom