Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo mnafanya Kosa walilofanya CHADEMA mwaka 2015. Mgombea anaeuzika kwa sasa ni Tundu Lissu

Mkuu serikali ya vyama vinavyoungana wanakaa na kukubaliana watakapochukua serikali wanapeana "positions " ili kuendesha serikali.unaweza kuangalia kwa mfano nchi ya Kenya.
 
Mkuu serikali ya vyama vinavyoungana wanakaa na kukubaliana watakapochukua serikali wanapeana "positions " ili kuendesha serikali.unaweza kuangalia kwa mfano nchi ya Kenya.

Lazima makubaliano hayo yawepo kabla ya uchaguzi mkuu, la sivyo kuna kuzinguana huko mbele ya safari

Pili ishu ya kuachiana majimbo ya ubunge nayo ni mtihani mwingine!
 
Kuna jambo la kitechniki linafanyika tusubiri mambo yataeleweka tu.
Aluta continua!
[emoji109][emoji110][emoji2935][emoji2936][emoji123]
 
Kuna kitu mnashindwa kuelewa Membe ni plan B endapo lissu ataletewa fitna
 

Wataunda serikali ya pamoja mbona hiyo rahisi kabisa, hakuna sheria inayomkataza Rais kuteua mbunge wa chama kingine kuwa Waziri kwenye serikali yake
 
Kama Lisu ndiye pekee anauzika,sioni ni nini kinachowaliza.

Sasa Membe anaathiri vipi mauzo ya Lisu kama ndiye pekee anayeuzika?

Anapunguza kura na kutoa nafasi kwa magufuli kushinda
 
Hivi nyie viumbe mnaamini mtashinda mbele ya hii tume na katiba iliyopo??

Daaah Huo muda wa kupiga kura bora nipige ulabu tuu huku na ruka debe la rege za luck Dube

Kura zinapigwa na wananchi siyo tume sasa wananchi wakishachagua kiongozi wanayemtaka tume kazi yake ni kutangaza tu na kura zinahesabiwa hadharani kila kituo
 
Anapunguza kura na kutoa nafasi kwa magufuli kushinda

Atapunguzaje kura? , kama kuna watakaompa kura basi maana yake wameona yeye ndo anayewafaa, Kama wangeona Lissu ndo anayewafaa basi wangempa huyohuyo Lissu in the first place.

Sioni mantiki ya kuwanyima wananchi chaguo wanalotaka, kwa kuwalazimishia option chache.

Wananchi wakikukubali watakuchagua tu hata kama kuna wagombea 100, watawaacha 99 wakupigie wewe kwa wingi zaidi
 
Kura zinapigwa na wananchi siyo tume sasa wananchi wakishachagua kiongozi wanayemtaka tume kazi yake ni kutangaza tu na kura zinahesabiwa hadharani kila kituo
Hapa umeongea point napigia msitari maneno "Wananchi wanayemtaka". Kwa hiyo wananchi wakikutaka basi watakupa kura tu hata kama kwenye karatasi za kura kuna wagombea 100
 
ACT hawana impact Tz bara but Zanzibar
 
Hakuna ujanja ujanja Safari hii kila mmoja ashinde mechi zake. Kila Chama kina haki ya kusimamisha wagombea sio CDM pekee yake. Huyo TL unaesema atashinda sijui atashindaje ambapo hataweza hata kupata wabunge 20?.
Chadema walijisahau kuwa Safari ya Kisiasa Ni long-term sio short term wakafukuza akina zito kabwe Kama mbwa na akina duni Haji ambao kipindi hiki wangewafaa

Sasa kila mtu ale jeuri yake

Safari Hakuna wa kukubali utapeli wa Chadema kwenye UKAWA 2015
 
ACT hawana impact Tz bara but Zanzibar
Sio kweli mbona Halmashauri ya Ujiji iko Chini ya ACT wazalendo ? Acheni kutapa tapa Chadema bara hakina ila Lowasa na Slaa ndio walikuwa na nguvu bara ya kufanya Chadema ishinde bara

Sasa hivi hakuna ndani ya Chadema wa kuipa Chadema ushindi hayupo
 

Mjomba unapigia mbuzi gitaa wakati hawezi kucheza, Zitto anajua anayeuzika kwa upande wa wapinzani ni Tundu na siyo Membe! Kama Membe hataachia bendera ya upinzani kubebwa na Tundu, ni wazi Rais Magufuli atapita kwa kishindo siyo chini ya 90% ya kura zitakazo pigwa! Ni mchezo wa 2015 wa kumshambulia Lowassa na kutangaza ni fisadi itajirudia na baada ya 28/10/2020 Mhe Membe atarudi nyumbani kama Mhe Lowassa!!! Yetu macho, Magufuli juu juu juu zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…