FAHAD KING
JF-Expert Member
- Sep 14, 2017
- 301
- 375
Wanabodi
Kwanza nimshukuru Mungu kwa kumaliza mfungo ilihali nina afya njema na furaha tele kuliko kawaida.Kweli naamini hadithi ya Mtume Muhammad (S.A.W) "Funga ni Afya".
Pia Eid Mubarak kwa Waislamu Wenzangu na Pia ambao sio Waislamu tuzide kudumisha upendo na ushirikiano kwani sisi si chochote si lolote kwa muumba.Kwa hakika sisi ni dhaifu sana.
Clarification na Background kidogo
Siasa ni kitu kipana sana.Ni kitu ambacho kinahitaji akili za ziada kuwin attention za wanajamii, kwa maana hiyo Siasa ni Mindfulness Game bila shaka sote tunafahamu hili.Yaani kwenye siasa bana dah!! We mchafue mwana ushinde game.Kila mtu analake jukwaani
Nakumbuka kuna Sister angu mwaka 2015 alikua anataka kua Mbunge wa Viti Maalumu kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) pia pembeni kulikua na shemeji ake yeye alikua anagombea Ubunge wa jimbo kupitia CHADEMA sasa Jukwaani wa CDM anamsema na kumdharirisha wa CCM bila sababu za msingi.Imefikia stage hakuna hoja inayojengwa zaidi ya Siasa za kuchafuana.
Leo wote wamekosa.Undugu hakuna kila kona kufyonzana.Ndugu wanakua maadui, marafiki wanakua wanafiki.Siasa inahitaji moyo sana.Ni wachache ambao wapo au wanataka kuongoza kwa niaba ya wananchi wao.Ni wachache sana ambao wapo kwa lengo la kupaza sauti za Wananchi wao.
Nachotaka kusema
Kuna kamsemo ka Waswahili kanasema "Jifunze kupitia historia ya mwenzako" japo sio rasmi.Au kale ka "Asie Funzwa na ***** Hufunzwa na Ulimwengu".Lengo lake ni nini?...Lengo ni kutahadharisha ACT Wazalendo kama kweli wanataka kua chama bora cha Ushindani.
Hakuna ambae hajui umuhimu kwa vyama bora vya Upinzani kwenye Serikali ya kidemokrasia kama hii.Ujengaji wa Hoja, pia kuibua masuala ambayo ni tija kwa Taifa zima.Mfano Sakata la Richmond,Sakata la Escrow pia Makenikia na hata Sakata ndege.Hii yote ni kua na Upinzani ulio imara kwenye kujenga nchi Bora.Chama Tawala inabidi itazame hili kwa jicho la kutaka Upinzani ili kuimarisha Ubora wa Chama Tawala kwa miaka mingi zaidi.
Juzi nimeshtushwa kidogo na tetesi za Chama Cha ACT Wazalendo kutaka kumkabidhi Mh Benard Membe adhma ya kugombea Uraisi mwaka 2020.Nimeshangaa kwanini bado ACT Wazalendo hawajajifunza toka kwa CDM yale waliofanywa mwaka 2015?...Hivi ni kweli wanania ya kuongoza Taifa kwa kumsimamisha aliekua KADA wa CCM kwa miaka 10-15 tena nyadhifa za kugombea Uraisi.Zitto umefikiria nini?...Au ni mimi tu fikra zangu nakosea kutazama hili jambo kwa namna ingine tena?🤔
Nawasiwasi pale nakufikiria huenda ni kweli Wapinzani hamjui mnachotafuta.Mwaka 2015 CDM ilimsimamisha Edward Lowassa.Kwa kweli Chama Tawala tuliwapelekesha puta kweli kwenye masuala ya kampeni.Nikaamini huenda Mwanga utakuja.Mwishoni mambo hayakua mazuri,tukakubali matokeo lakini ghafla mzee huyooo karudi zake CCM.SIASA ni MINDFULNESS GAME.SIASA ni kuchezeana akili kisha unaachwa kwenye mataa
Ukweli ni kwamba huwezi ukasimamisha KADA wa CCM kugombea Uraisi dhidi ya Chama Chake kilichomlea CCM.Huwezi labda kama unataka tu Chama Chako nacho kitoe mgombea kiti cha Uraisi pasipo kuweka Ushindani kwa wananchi.
Sitaki kuongea Mengi..ACT jifunzeni kwa CDM ya mwaka 2015
Msirudie makosa 2020
Eid Mubarak