Ccm kama chama hakina uwezo wa kuangamiza chama chochote kisiasa, kwani chama chochote cha siasa huangamiza chama kingine kwa ushawishi wa sera na hoja. Lakini tunaona wazi sasa hivi wapinzani hawashindani na ccm, bali wanafanyiwa uhayawani, ukatili na rafu za wazi na vyombo vya dola, mahakama, bunge na taasisi nyingine za kimamlaka. Ccm kama chama wamebaki kwenye propaganda mfu tu.
Madaraka ya rais yanayotumika vibaya ndio imegeuzwa kuitwa uimara wa ccm! Kwa mtu yoyote mwenye ufahamu wa kawaida kabisa, anajua sasa hivi hakuna ushindani wa kisiasa, bali kuna siasa chafu dhidi vya wapinzani. Ccm kwa sasa imebaki kutumia shuruti kukubalika, kwakuwa mwenyekiti wake ana kofia ya urais anayoweza kuitumia vibaya. Kwa ajili ya ulevi wa madaraka, sasa hivi anajijengea kinga ya kutoshtakiwa yeye na wenzake wanaotumia madaraka vibaya. Sasa kama mwenyekiti anasaka kinga ya kutoshtakiwa kwa makosa anayoyafanya sasa, huo uimara wa ccm uko wapi?