Nguruka
Senior Member
- Dec 6, 2006
- 189
- 129
Nini maana halisi ya Barua hii ya Chama cha ACT Wazalendo waliyomuandikia msajili wa Vyama vya Siasa kujibu Tuhuma dhidi yao.
Ni dhahiri kuwa ACT imekosa imani na mtu waliomsimamisha kuwania Kiti cha Rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu nchini Tanzania. Na hili linaweza kuwa funzo kwa baadhi ya Vyama vya Siasa kuacha kupapatikia wagombea wanaotoka chama kimoja kwenda kingine pasipo kupima nguvu yao kisiasa na ukubalikaji wao katika jamii.
Membe aliyefukuzwa uanachama ndani ya Chama cha Mapinduzi alijiunga na CCM na kuwaaminisha kuwa anaweza kufurukuta na ananguvu kubwa ya kushinda Kiti cha rais lakini baada ya taarifa ya hivi karibu ya Mwenyekiti wa Chama hicho na Mgombea Kiti cha Urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad inaonesha chama hicho kukosa aminani nane na hiovyo kuamini kwa Mgombea wa Chadema.
Na hii inadhihirishwa na hata kasi ya mgombea huyo kufanya mikutano ya kampeni kama ambavyo aliahidi kua akianza atatikisa. Swali ambalo huenda wewe na mimi tunajiuliza hivi sasa ni juu ya hatma ya mgombea wa ACT Wazalendo.
Je, Wanamaanisha kuwa mgombea wao waliomsimamisha Ndugu Bernard Kamilius Membe bado anagombea lakini hawana Imani nae kua anaweza kufurukuta hivyo wameamisha imani yao kwa Chadema.
Nasema Membe Bado ni Mgombea wa ACT Wazalendo sababu hadi hii leo Tume ya Uchaguzi hatujaisikia ikitoa taarifa juu ya kujiengua kwea Mgombea huyo wa ACT Wazalendo.
ACT-Wazalendo wameikimbia hoja ya Msajili kua wao wanampigia chapuo Tundu Lissu na barua hii wanaonesha pia kukana kumuombea kura Tundu lakini imani yuao Wanaamini kua Tundu atashinda.