ACT Wazalendo: Ratiba ya Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ) iheshimiwe

ACT Wazalendo: Ratiba ya Ligi Kuu ya Zanzibar (PBZ) iheshimiwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2025-04-03 at 12.11.15_d3cf6f83.jpg

WhatsApp Image 2025-04-03 at 12.11.15_ba388578.jpg
RATIBA YA PBZ PREMEIR LEAGUE IHESHIMIWE
Shirikikisho la Soka la Zanzibar ZFF lilikuwa limepanga Ligi Kuu ya PBZ iendelee kuchanja mbuga kuanzia Aprili 5, 2025 na kutafuta vidume vya Zanzibar ili kuweza kuwakilisha katika michuano ya vilabu barani Afrika ambapo bado ZFF ina uwanachama Shirikishi.

Hadi sasa timu ya Mwembe Makumbi City inaongoza, PBZ Premier League ikiwa na pointi 41 baada ya mizunguko 20 na kufuatiwa kwa karibu na timu ya Mmlandege FC yenye pointi 38. Ligi hiyo kwa sasa iko nusu bin nusu.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ilikuwa na mazungumzo na ZFF kuwa ligi hiyo itakapoanza tena baada ya kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan, itachezwa katika viwanja vya Amani, Unguja na kule Gombani Pemba na sio tena katika viwanja vya dharura vya Kairo, Kaskazini Unguja na Kinyasini, Kaskazini Pemba.

Ligi Kuu ya Zanzibar ilihamia katika viwanja hivyo duni, vinavyohatarisha afya za wachezaji na visivyotimiza viwango kuanzia Novemba 4, 2024 pakiwa hakuna ahadi rasmi ya lini itarudi katika viwanja vyenye vipimo na ubora unaokubalika.

Awali tulielezwa kwamba matengenezo ya viwanja vya Gombani na Amani yalikuwa na madhumuni ya Zanzibar kujiweka sawa kutokana na uwenyeji wa Tanzania wa michuano ya CHAN ambayo ni maalum kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani za Afrika.

Pamoja na kutangazwa kuwa Serikali itatumia kiasi cha dola za Kimarekani, 6,300,000 ambazo ni sawa na kiasi cha Shilingi za Tanzana 16,672,541,760 Amani (New Amani Complex) na kwa upande wa Kiwanja cha Gombani fedha zitakazotumika ni Dola za Kimarekani 4,250,000 ambazo ni sawa na kiasi cha Shilingi za Tanzana 11,247,349,600, ikiwa ni juu ya fedha nyingi zilizokwisha kutumika kujenga/kukarabati viwanja hivyo, zipo taarifa zimekuwa zikisema kuwa Shirikisho la Soka Afrika CAF limefelisha matengenezo hayo na kutoa maelekezo mapya ya kutengeneza/kukarabati viwanja hivyo.

ACT Wazalendo tuliwahi kuhoji juu ya matumizi ya ujenzi ule, ulioitwa uboreshaji, ambayo hayakupitia utaratibu wa kawaida wa matumizi ya Serikali na kuitaka Wizara inayohusika kutoka hadharani kueleza kwa ujumla viwanja hivyo hadi sasa vimegharimu fedha za umma kiasi gani.

ACT Wazalendo, tunazo taarifa kwamba, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ilikuwa imefanya mawasliano na ZFF kuwa Ligi ya PBZ ingeweza kuendelea kuanzia April 5, 2025 katika viwanja vya Amani na Gombani, lakini kwa taarifa ya Bodi ya Ligi Zanzibar ya tarehe 01/04/2025 inaonekana bado hakuna uhakika wa ligi hiyo kurejea kwa wakati muafaka, kutokana na kutokabidhiwa viwanja hivyo, jambo ambalo linaliweka pabaya Shirikisho hilo kwa klabu zake za Ligi Kuu na wadhamini wake.

Inajulikana pia ndani ya kipindi cha miezi ya karibuni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga kiwanja mchanganyiko cha michezo hapo Maisara na ndani yake vikiwemo viwanja viwili vya kuchezea soka au mpira wa miguu, na inapaswa viwanja hivyo vitumike ili Ligi Kuu ya Zanzibar imalize kwa wakati.
Msimamo wa ACT Wazalendo:

1.Ligi Kuu ya PBZ irejeshewa heshima yake kwa kurudishwa katika viwanja stahiki ili pia kulinda afya za wachezaji

2. Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo itoe kwa wakati viwanja hivyo kama ilivyojifunga hapo awali ili Ligi Kuu ya PBZ ianze mara moja ili kuheshimu program za waalimu za matayarisho ya Ligi hio.

3. Wizara itoke hadharani kuelezea ni makosa gani yaliotolewa na CAF kuhusu kiwanja cha Amani na marekebisho yaliopendezwa.

4.Serikali ieleze hatua gani zitachukuliwa kwa mkandarasi ambayo kila uchao anawatia hasara wananchi wa Zanzibar na fedha kiasi gani za umma zitatumika kukamilisha marekebisho yaliopendezwa na CAF.

5.ACT Wazalendo inasisitiza kuwa soka na michezo kwa jumla, ni kipaumbele chake kwa kuwajenga vijana na pia kujenga taifa la wanamichezo kwa kuamini kuwa michezo ni sekta muhimu ya ajira.

Imetolewa leo, tarehe 03/04/2025 na,
Ally Saleh Alberto
Msemaji wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
0715430022
 
Zanzibar awamu hii usipotajirika bas ww kilaza, watu wanatafuna pesa sio mchezo sijui Kwa vile zinatoka Kwa mama Yao ndio maana hawana uchungu nazo?
 
Back
Top Bottom