Zanzibar 2020 ACT-Wazalendo: Taarifa ya njama na mipango ovu ya tume ya uchaguzi (ZEC) wakishirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM

Zanzibar 2020 ACT-Wazalendo: Taarifa ya njama na mipango ovu ya tume ya uchaguzi (ZEC) wakishirikiana na Chama cha Mapinduzi CCM

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
TAARIAFA KWA UMMA

Ndugu waandishi wa Habari. Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenye ezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi kwa kutujaalia tukawa katika hali ya uzima wa Afya na muda huu kujumuika pamoja hapa. Ingawa tumewaita muda mfupi uliopita, lakini bado mmejali na kuitikia wito wetu huu na kuja hapa ili kutusikiliza na kutupelekea taarifa zetu hizi kwa umma wa Wazanzibari na wapenda demokrasia ulimwenguni.

Ndugu waandishi wa habari, kama mnavyojua kwamba leo ndio siku ya mwisho ya Uchukuaji na Urejeshaji wa Fomu za kuomba kuteuliwa katika nafasi za Urais wa Zanzibar, Uwakilishi na Udiwani kwenye Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC). Wagombea wetu wa nafasi hizo tayari wamerudisha fomu zao.

Kilichotufanya tuwaite ni kwamba tunazo taarifa za kuaminika za mipango na njama ovu zilizoandaliwa na kuratibiwa kwa pamoja kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na katika baadhi ya maeneo kuwahusisha maofisa waandamizi wa Serikali katika taasisi mbali mbali. Njama hizo ni za kuwawekea pingamizi wagombea wetu katika majimbo ambayo CCM wana uhakika hawawezi kushinda, lengo likiwa ni kuwaondoa wagombea wetu katika Uchaguzi kama ambavyo wamefanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Mapingamizi hayo ni katika majimbo yote kumi na nane (18) ya Pemba, lakini hasa mkakati wao na njama zao wakizitilia mkazo kwa wagombea wafuatao:-

1. Abubakar Khamis Bakary – Jimbo la Pandani
2. Said Ali Mbarouk - Jimbo la Gando
3. Omar Ali Shehe - Jimbo la Chake Chake
4. Seif Khamis Mohamed - Jimbo la Mkoani
5. Hija Hassan Hija - Jimbo la Kiwani
6. Subeti Khamis Faki - Jimbo la Micheweni
7. Hamad Masoud Hamad - Jimbo la Ole

Kwa upande wa Unguja, mpango huo pia umepangwa kutekelezwa katika Wilaya ya Kaskazini A, Wilaya ya Magharibi A na B na wilaya ya Mjini, laki hasa mkakati wao na njama zao wakizitilia mkazo kwa wagombea wafuatao:-

1. Nassor Ahmed Mazrui - Jimbo la Mwera
2. Juma Duni Haji - Jimbo la Mtoni
3. Nassor Ali Amour - Jimbo la Chumbuni
4. Ismail Jussa Ladhu - Jimbo la Malindi
5. Abdillah Jihad Hassan - Jimbo la Mwanakwerekwe
6. Hassan Jani Massoud - Jimbo la Nungwi
7. Dr. Haji Ali Mbarouk - Jimbo la Tumbatu
8. Haji Mwadini Makame - Jimbo la Kijini

Ndugu waandishi wa Habari, katika mpango huo tunazo taarifa za kuaminika katika Jimbo la Chumbuni za kumtumia Ndugu Khamis Jabu Mohamed ambaye amefukuzwa katika chama chetu kwa kumkabidhi fomu ya Uwakilishi wa Jimbo la Chumbuni ili kumuondoa Mgombea wetu halali, Ndugu Nassor Ali Amour.

Ndugu waandishi wa Habari, tunawataka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kuacha mara moja kupanga mipango hii miovu ya kutaka kuingiza nchi katika machafuko yasiyokuwa ya lazima kwa kuendelea kutumika na kukibeba Chama Cha Mapinduzi wakijua fika kwamba kwa wakati tulionao CCM hakisaidiliki tena kwani wananchi wameshakikataa na uthibitisho wa hilo ni Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambapo walishindwa kwa aibu.

Hitimisho

Ndugu, Waandishi wa Habari tunaitahadharisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa kutaka kuwaondosha wagombea wetu kwa mipango na makosa ya kutengeneza. Tunaitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kwanza wajitathmini wao, ikiwa Tume nzima ya Uchaguzi inayoongozwa na Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, na Makamishna ambao wengine ni Majaji wa Mahakama Kuu, kufanya makosa ya kutokuwepo kwa sehemu nzima ya TAMKO LA UTHIBITISHO WA WADHAMINI katika fomu ya uteuzi wa Uwakilishi (na kulazimika kutoa nakala za photocopy leo baada ya Chama chetu cha ACT Wazalendo kuwatanabahisha suala hilo kwa barua jana), wanawezaje kuja kuwaondosha wagombea wetu kwa hujuma au makosa ya kutengeneza?

Tunaitaka Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ifanye kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za Uchaguzi bila ya kumbeba na kumpendelea yoyote yule na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa kuwapa kile walichokichagua. Hatutakubali wala kuvumilia njama zozote zile ovu zinazoratibiwa kuona zinawaondosha wagombea wetu


Nassor Ahmed Mazrui
Naibu Katibu Mkuu, ACT-Wazalendo

Zanzibar
09/09/2020.
 
Huku ni kutapa tapa kwa mfa maji, ingekua kweli CCM wanawaondoa wapinzani sehem ambazo hawawezi kushinda basi wabunge wa chadema wote wanaotetea nafasi zao wangeenguliwa bara coz wana nafasi kubwa ya kushinda kuliko wagombea wa CCM.
 
Nadhani uthibitisho utasaidia zaidi jamii kujua na wahusika kujiona mipango yao ipo naked.
 
Hao ZEC toka Jecha alivyochomoaga betri kipindi kile naonaga ni mashetani tu.

NEC huwa wanajitahidi wizi wa standard kidogo hawa Jecha organization wanachofanya ni unyang'anyi
 
Mgombea urais was CCM ana hali Sana jumapili aliachiwa msikiti baada ya kuingia waumini wakasema hawawezi kuswali na mnafiki, Sasa kakimbili mitaani kijichanganya, Mpaka aibu.

IMG_20200909_140757.jpg
 
Chama cha Magufuli a.k.a ccm itazizma hilo zote za chama cha mapinduzi
 
Huku ni kutapa tapa kwa mfa maji, ingekua kweli CCM wanawaondoa wapinzani sehem ambazo hawawezi kushinda basi wabunge wa chadema wote wanaotetea nafasi zao wangeenguliwa bara coz wana nafasi kubwa ya kushinda kuliko wagombea wa CCM.
Tume irudishe wagombea wote, jukumu lao ni kusimamia uchaguzi siyo kupanga matokeo kwa kupendelea CCM.

Kama mtu ni raia wa Tanzania na ana umri wa miaka 18, na anajua kusoma na kuandika arejeshwe agombee wananchi ndio tuamue.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Toka Jecha afanye yake 2015, hiyo Zec imepoteza imani kwa wadau wake (vyama vya upinzani).
 
CCM ya sasa ina Hali ngumu Sana.Wameamua liwalo na liwe lazima washinde!
 
Huku ni kutapa tapa kwa mfa maji, ingekua kweli CCM wanawaondoa wapinzani sehem ambazo hawawezi kushinda basi wabunge wa chadema wote wanaotetea nafasi zao wangeenguliwa bara coz wana nafasi kubwa ya kushinda kuliko wagombea wa CCM.
CCM wanajua pale kwenye sanduku la KURA watafanya nini. Hao wagombea wa UPINZANI wachache sana watapewa ushindi ili kuhalalisha UHARAMIA mwingine kitaifa.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Tume irudishe wagombea wote, jukumu lao ni kusimamia uchaguzi siyo kupanga matokeo kwa kupendelea ccm.

Kama mtu ni raia wa Tanzania na ana umri wa miaka 18, na anajua kusoma na kuandika arejeshwe agombee wananchi ndio tuamue.
Vigezo vikubwa ni
1 uraia
2 umri
3 kujua kusoma nakuandika
4 kuwahi kufanya makosa
Vilivyobaki niupuuzi mtupu hata hao waicho chama wanaojifanya waondio mafundi wa kujaza form naowanakosea lakini hakuna wa kumfunga paka kengere tupaze sauti wananchi nchi hii sio yachama fulani niyetu wote naamani niyasisi wote tuilinde
 
Yaani taarifa za aina hiyo mnazipata nyie tu.
 
Nidhahiri kabisa sisiem inataka kuleta machafuko na utakuta kuna mashetani yanafurahia kabisa na kushangiria, meno yote nje..

Wanafanya hivyo kwa thamani duni kabisa.. et elfu 7 kwa siku, kanga za vyama nk

DHULMA HAIDUMU NAWAAMBIA
 
Back
Top Bottom