GE2025 ACT Wazalendo Tawi la Mafifi Lamfuta Uanachama Monalisa Joseph Ndala

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kikao cha Kamati ya Uongozi ACT Wazalendo kilichofanyika Tarehe 28 Agosti, 2025 Iringa Mjini, Kata ya Kihesa, Mtaa wa Mafifi, kimepitia na kufanya ukaguzi wa hali za uhai wa Wanachama wake wa Tawi kwa ujumla na kubaini kuwa umepoteza sifa za kuwa Mwanachama halali na hai wa Chama cha ACT Wazalendo kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015, Toleo la Mwaka 2024, Ibara ya 8 (2) (a) (b) na Ibara ya 13 (1) (c) (d) pamoja na Ibara ya 97 (b) (d).

Kwa mujibu wa Ibara ya 97 (1) (d), Kamati ya Uongozi ya Tawi imejiridhisha kuwa wewe Monalisa Joseph Ndala umeshindwa kutekeleza matakwa ya Katiba ya Chama na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo.

Kwa barua hii tunakujulisha rasmi kuwa kuanzia leo Tarehe 28/10/2025, Kamati ya Uongozi ya Tawi la Mafifi tumekuondoa katika orodha ya Wanachama wake katika regista ya Tawi na Kadi Namba 0000245 iliyokuwa imeandikishwa kwa jina lako ipo wazi na tumeitaarifu Idara ya Oganaizesheni, Uchaguzi na Wanachama ya Chama Taifa ili iweze kutolewa kwa Mwanachama mwingine.

Pamoja na salamu za Chama: ACT Wazalendo, Taifa
View attachment 3457732
 
Eeh wajitafakari Bana, maana itayumkinika vipi binti mzabalijadi mla yombiyombi kumshikia korofindo mgonjwa wa shetri
 
Hiki chama kama ni cha machizi, yaan mtu awe na akili zake timamu ajiunge na hiki chama kweli, Mpina ametudhalilisha kugombea urais bora angegombea ubunge, yaan mijitu iliyopo humu ACT kama punguani vile sijui inawaza siku moja itatawala Taifa
 
Project za CCM zina maigizo mengi kutusahaulisha ila bado hatudanganyiki.

No reforms no election.

Free Lissu.
 
Ha
Kikao cha Kamati ya Uongozi ACT Wazalendo kilichofanyika Tarehe 28 Agosti, 2025 Iringa Mjini, Kata ya Kihesa, Mtaa wa Mafifi, kimepitia na kufanya ukaguzi wa hali za uhai wa Wanachama wake wa Tawi kwa ujumla na kubaini kuwa umepoteza sifa za kuwa Mwanachama halali na hai wa Chama cha ACT Wazalendo kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ya Mwaka 2015, Toleo la Mwaka 2024, Ibara ya 8 (2) (a) (b) na Ibara ya 13 (1) (c) (d) pamoja na Ibara ya 97 (b) (d).

Kwa mujibu wa Ibara ya 97 (1) (d), Kamati ya Uongozi ya Tawi imejiridhisha kuwa wewe Monalisa Joseph Ndala umeshindwa kutekeleza matakwa ya Katiba ya Chama na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo.

Kwa barua hii tunakujulisha rasmi kuwa kuanzia leo Tarehe 28/10/2025, Kamati ya Uongozi ya Tawi la Mafifi tumekuondoa katika orodha ya Wanachama wake katika regista ya Tawi na Kadi Namba 0000245 iliyokuwa imeandikishwa kwa jina lako ipo wazi na tumeitaarifu Idara ya Oganaizesheni, Uchaguzi na Wanachama ya Chama Taifa ili iweze kutolewa kwa Mwanachama mwingine.

Pamoja na salamu za Chama: ACT Wazalendo, Taifa
View attachment 3457732
Hao ndiyo wapinzani wanaodai haki na demokrasia. Wacha tubaki na CCM yetu huko ni majanga zaidi
 
Back
Top Bottom