Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo: Tunaendelea kutafuta haki ya wagombea wetu wa ubunge na udiwani wa walioenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi

Uchaguzi 2020 ACT Wazalendo: Tunaendelea kutafuta haki ya wagombea wetu wa ubunge na udiwani wa walioenguliwa na wasimamizi wa uchaguzi

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2014
Posts
631
Reaction score
1,577
Na Mwandishi Wetu

CHAMA cha ACT–Wazalendo kimesema kinaendelea kutafuta haki ya wagombea wake wa nafasi za ubunge na udiwani ambao wameenguliwa kihuni na wasimamizi wa uchaguzi kwa kufuata taratibu zote za kisheria.

Hayo yamesemwa leo Agosti 27, 2020 jijini Dar es Salaam na Meneja wa Kampeni Taifa wa chama hicho, Emmanuel Lazarusi Mvula ambapo amesema uamuzi huo wa dhuluma na mapingamizi ya ovyo umefanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake.

Meneja huyo wa kampeni amesema kutokana na uhuni huo wa CCM kutaka kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa goli la mkono, chama kimewaagiza wagombea wake wote ambao wameenguliwa nchi nzima kuhakikisha wanakata rufaa kulingana na nafasi husika na wale ambao rufaa zao hazijaamuliwa waendelee kuvuta subira wakati zinafanyiwa kazi.

“Aidha maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi kuwakata wagombea wetu kwa kiwango cha kutisha yana dalili za waziwazi za kuwapo matumizi ya rushwa, hivyo tunaitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza mienendo ya Wasimamizi hao.

“ACT-Wazalendo tunaamini uovu huu uliofanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi utarekebishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwarejesha wagombea wetu wote kuendelea na mchakato wa uchaguzi kwa mujibu wa sheria.

“Zaidi chama kinalaani na kukemea uhuni huo na tunaendelea kufuata taratibu zote za kisheria kuhakikisha haki inatendeka na kama ikishindikana tutachukua hatua ambazo tusingependa kufika huko, lakini wakitulazimisha kufika huko nasi tutalazimika kuwafundisha Watanzania namna ya kudai haki yao.”alisisitiza Mvula.

Meneja huyo wa kampeni alikisihi Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali yake kwamba wawaache Watanzania wachague viongozi wanaowataka bila kuingiliwa.

Mwisho
 
Back
Top Bottom