ACT Wazalendo: Tunalitaka jeshi la polisi limuachie huru Wakili Madeleka

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha ACT Wazalendo kinakemea vikali kukamatwa kwa Wakili Peter Madeleka jioni ya jana Agosti 14, 2026, nje ya Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi akiwa anatekeleza majukumu yake. Polisi wamemkamata kwa kile wanachodai kudharau amri ya Mahakama Kuu.

  • Kukamatwa kwa wakili akiwa katika majukumu yake ni tishio kwa uhuru wa kitaaluma wa mawakili,ukiukwaji wa wazi wa sheria zinazotoa uhuru wa kujieleza na wananchi kupata habari. Wakili Madeleka amekuwa mstari wa mbele kupigania haki, utawala wa sheria na Katiba Mpya.

Mapema jana baada ya kutoka mhakamani, alizungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa amri inayowazuia mawakili kuzungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama ni batili na haina msingi wa kisheria, huku akitaka itajwe sheria inayokataza jambo hilo.

Aidha, alihoji mantiki ya mahakama kuzuia mawakili wakati yenyewe ina chombo cha habari kinachorusha matukio ya mahakamani. Pia alikosoa utaratibu wa makamanda mbalimbali wa polisi kuwakamata watuhumiwa na kuwapeleka mbele ya vyombo vya habari, huku wakiwaita wahalifu kabla hawajafikishwa mahakamani. Alihoji iwapo kufanya hivyo hakuathiri mwenendo wa kesi na kwa nini mahakama iko kimya.

ACT Wazalendo tunaona huu ni mwendelezo wa mihimili ya dola kuchukua mwelekeo wa ukandamizaj. Tumeona Serikali ikidhibiti uhuru wa habari, Bunge likidhibiti wabunge, na sasa mahakama ikidhibiti mawakili wanapouhabarisha umma.

Hii ni hali ya hatari, watanzania tunapaswa kuamka na kupinga mwenendo huu na kudai uhuru kamili. Uhuru huo utapatikana kupitia katiba mpya ya wananchi.

Soma Pia:

Tunatoa wito kwa Jeshi la Polisi kumwachia huru bila mashart

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…