Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo wa Jimbo la Tunduru Kaskazini mkoani Ruvuma, Yasin Mohamed Mawila, ametoa onyo kali dhidi ya jaribio lolote la udanganyifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.
Akizungumza Jumapili, Novemba 24, 2024, kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika Kijiji cha Ligunga, Kata ya Ligunga, Jimbo la Tunduru Kaskazini, Mawila amewaonya vikali wale wanaopanga kutumia mbinu za kihuni ili kuvuruga uchaguzi huo.
Mawila amedai kuwa kuna mpango wa baadhi ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupiga kura za mapema na kupewa karatasi zaidi ya moja za kupigia kura ili kuongeza kura kwa njia ya udanganyifu. Amesisitiza kuwa ACT Wazalendo haitakubali vitendo hivyo na akaonya vikali wale watakaobainika kufanya udanganyifu huo.
"Watu wa CCM kama mko hapa, kuna vijana wakiume na wakike wamepangwa kupiga kura za mapema na kwenye upigaji wa hizo kura, watapewa karatasi zaidi ya moja kwenye kutumbukiza kwenye kiboksi cha kupigia kura. Wewe utakayetumwa kufanya jambo hilo, tukikubaini, wewe utapigwa kama wezi wengine na utapigwa moto. Hakuna mtu tutakayemchekea, tukikushika na makaratasi mengi utapigwa mpaka kufa, tumechoka chaguzi zote sisi tuwe tunalia tu, safari hii watalia wao," amesema Mawila kwa msisitizo.