Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Dorothy Semu, amesema kuwa Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, haina nina ya dhati ya kutimiza ahadi za maridhiano, kwa kuwa vyombo vya dola bado vinatumia mabavu kukandamiza hoja za msingi za vyama vya Upinzani, Kukamata wanasiasa wa Upinzani na kuwapa kesi za uhaini kwa lengo la kuwakatisha tamaa watanzania
Aidha Ndugu Semu amesema nguvu hizo za vyombo vya dola zinazotumika dhidi ya wapinzani, inadhihirisha namna Serikali na Chama tawala walivyokuwa maadui wa Demokrasia, na kwamba ACT Wazalendo haitakubali hofu hiyo iwe silaha ya kuwanyanyasa na kuwakandamiza wananchi, kudai haki zao za msingi na kwamba wataupinga ukandamizaji wa aina yoyote kwa uasi wa haki, uasi wa wajibu na uasi wa imani kuhakikisha demokrasia ya kweli inapatikana.
Ndugu Dorothy Semu ametoa kauli hiyo, leo tarehe 12, April 2025, wakati akihutubia katika Kongamano la Operesheni Linda Demokrasia lililofanyika katika mji Mdogo wa Mlowo Mbozi Mkoa wa Songwe, ikiwa ni Kongamano la nne la Chama chetu ikitanguliwa na mengine matatu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Lindi na Kigoma
"ACT Wazalendo tunawajua maadui wa demokrasia. Mtaji wao mkubwa ni hofu - kuwatisha Watanzania, kuwavunja moyo, na kuwafanya wakate tamaa. Lakini leo, mbele yenu, nasema wazi, hatutakubali hofu iwe silaha yao! Tutapinga ukandamizaji kwa uasi wa haki, uasi wa wajibu, uasi wa imani yetu katika demokrasia ya kweli"
Ndugu Semu alitumia Kongamano hilo kumpongeza Mwenyekiti Taifa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ndugu Tundu Lissu, kwa kusimama imara dhidi ya mifumo kandamizi na kusema kukamatwa kwake kwa kutumia neno "uasi" ni jaribio la kutaka kufunga mdomo wa haki.
Aliitaka Serikali na Chama tawala kuacha kuuzuia ukweli kwa kuwa hakuna aliyewahi kushindana na ukweli na kufanikiwa na kwamba mashtaka dhidi ya Tundu Lissu yataendelea kutupa nguvu zaidi ya kuendeleza mapambano badala ya kukataa tamaa.
Alitumia Kongamano hilo la Operesheni Linda Demokrasia, kusisistiza madai ya msingi Sita ya ACT Wazalendo, yanayopaswa kutekelezwa ikiwa kuna utashi wa kisiasa kuwa ni:

- Makamishna wa Tume ya Uchaguzi Wajiuzulu sheria, ili kurejesha imani katika uchaguzi wetu. na wateuliwe wapya kwa mujibu wa
- Mawakala wa Vyama wawe Huru matokeo bila vizuizi. wasitishwe, wawe na haki ya kupata fomu za
- Wagombea Wasienguliwe kwa Sababu za Kipuuzi makosa ya kiufundi yarekebishwe kwa haki, sio kuenguliwa.
- Kura Feki Zidhibitiwe uchaguzi uwe safi, bila wizi wa kura.
- Wakurugenzi wa Halmashauri Wasiwe Wasimamizi wa Uchaguzi uchaguzi uendeshwe na watu wa kujitegemea.
- Vyombo vya Ulinzi Visihusike na Uchaguzi polisi na jeshi viwe vya kulinda, sio kutisha wananchi.