Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
ACT Wazalendo ilimjulisha rasmi Waziri wa TAMISEMI ambaye ndiye Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huu kupitia barua ya Katibu Mkuu ya tarehe 20 Oktoba 2024 yenye Kumbukumbu Namba ACT/HQ/OFKM/011/VOL.III/256. Barua yetu ilifuatia barua ya Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ya tarehe 14 Oktoba 2024 yenye Kumb. Namba CCB.126/215/01/85 ambayo ilielekeza kuwa vyama vya siasa vitaamua vyenyewe ngazi za udhamini za wagombea. Kwa masikitiko makubwa, kwenye baadhi ya maeneo, kupitia mapingamizi yaliyowekwa na wagombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya wagombea wetu, Wasimamizi Wasaidizi wamewaengua wagombea wetu kwenye baadhi ya maeneo hayo kwa kigezo cha kudhaminiwa na ngazi kata.
Ni jambo la kustaajabisha kuwa katika nchi moja, wapo baadhi ya wagombea wetu wameteuliwa kwa kudhaminiwa na ngazi ya kata lakini wengine wengi wametenguliwa. Waziri Mchengerwa amekubali vipi maelekezo yake kupuuzwa?
WITO WETU:
Tunamtaka Waziri wa TAMISEMI Ndugu Mohamed Mchengerwa kutoka hadharani na kuwataka Wasimamizi wa Uchaguzi kuwarejesha wagombea wetu wote walioenguliwa kwa kigezo hiki kwani kuenguliwa kwao ni dharau ya dhahiri kwake kama Mamlaka ya Uchaguzi. Uvumilivu wetu una kikomo.
Rai hii imewasilishwa pia kwa maandishi kwa barua ya Katibu Mkuu jana tarehe 10 Novemba 2024.
Imetolewa na;
Rahma Mwita,
Msemaji wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo. Novemba 11, 2024