PostGE2025 ACT Wazalendo waikataa ripoti ya Jaji Chande. Wasema Tume haina Uhuru, ni chombo cha kulinda wahusika

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa msimamo wake wa awali kufuatia kupokea taarifa ya Tume ya Uchunguzi wa Mauaji ya Oktoba 2025 iliyowasilishwa leo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Aprili 23, 2026, chama hicho kimesema kinasimama imara katika msimamo wake wa awali wa kukataa kile kinachoitwa Tume ya Jaji Chande, kikidai kuwa tume hiyo haina uhuru wala uaminifu wa kutosha kutenda haki kwa wahusika wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, ripoti iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, ina hitimisho ambalo tayari lilitarajiwa kutokana na mwenendo wa tume hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Chama hicho pia kimetoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika matukio ya Oktoba 29, kikisisitiza kuwa haki na ukweli vinaweza kupatikana tu kupitia uchunguzi huru, wa kuaminika na ulio wazi kwa umma.

Aidha, ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuundwa kwa tume nyingine ya uchunguzi, kikidai kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma na kuchelewesha upatikanaji wa haki kwa wahanga.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kimerudia wito wake wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa chini ya taasisi kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika au Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

ACT Wazalendo kimesema huu ni msimamo wake wa awali na kitaendelea kutoa maelezo ya kina baada ya kupitia ripoti hiyo kwa undani ndani ya vikao vya chama vitakavyofanyika hivi karibuni.
1776968639334.jpg
 
Hawa nao hawaeleweki, huku wanataka kule hawataki, sijui lao ni lipi, wachague upande mmoja ama sivyo wachague kufa katikati wakiwa vuguvugu, baadae tuwatapike.
 
Chama cha ACT Wazalendo kimetoa msimamo wake wa awali kufuatia kupokea taarifa ya Tume ya Uchunguzi wa Mauaji ya Oktoba 2025 iliyowasilishwa leo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa Aprili 23, 2026, chama hicho kimesema kinasimama imara katika msimamo wake wa awali wa kukataa kile kinachoitwa Tume ya Jaji Chande, kikidai kuwa tume hiyo haina uhuru wala uaminifu wa kutosha kutenda haki kwa wahusika wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa ACT Wazalendo, ripoti iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman, ina hitimisho ambalo tayari lilitarajiwa kutokana na mwenendo wa tume hiyo tangu kuanzishwa kwake.

Chama hicho pia kimetoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika matukio ya Oktoba 29, kikisisitiza kuwa haki na ukweli vinaweza kupatikana tu kupitia uchunguzi huru, wa kuaminika na ulio wazi kwa umma.

Aidha, ACT Wazalendo kimeeleza wasiwasi wake kuhusu taarifa za kuundwa kwa tume nyingine ya uchunguzi, kikidai kuwa hatua hiyo ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma na kuchelewesha upatikanaji wa haki kwa wahanga.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kimerudia wito wake wa kufanyika kwa uchunguzi huru wa kimataifa chini ya taasisi kama Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika au Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

ACT Wazalendo kimesema huu ni msimamo wake wa awali na kitaendelea kutoa maelezo ya kina baada ya kupitia ripoti hiyo kwa undani ndani ya vikao vya chama vitakavyofanyika hivi karibuni.
View attachment 3578191
Screenshot_20260424-122929~2.png
 
Inashangaza sana CCM inatoa report yenyewe halafu inajipinga...
Hapo lengo ni kutaka kuwaingiza mtegoni wapambania haki na vyama vingine vya upinzani.
 
Back
Top Bottom