GE2025 ACT wazalendo walichokifanya kule Zanzibar 2015 baada ya kumeguka CUF wanaweza kukifanya tena 2025 huku bara baada ya kumeguka CCM na CHADEMA

GE2025 ACT wazalendo walichokifanya kule Zanzibar 2015 baada ya kumeguka CUF wanaweza kukifanya tena 2025 huku bara baada ya kumeguka CCM na CHADEMA

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,751
Siasa ni kama mchezo wa karata. Mjanja anayeweza kuzicheza karata zake vizuri kwa kawaida huibuka mshindi.

Zitto Kabwe ni hodari wa kuucheza huo mchezo. Anajua kuwa kumeguka kwa vyama vikuu vya siasa kuelekea uchaguzi mkuu vinatoa fursa za kuimarisha chama chake.

Mwaka 2015 chama cha CUF kilimeguka kwa kumtosa Maalim Seif ambaye alikuwa na ushawishi mkubwa huko Zanzibar. Yeye na wafuasi wake wakavua tanga na kutinga ACT wazalendo. Matokeo yake kila mtu anayajua. ACT ndiyo chama kikuu cha upinzani huko Zanzibar.

Mwaka huu chadema na ccm vimemeguka. ACT wazalendo wamechukua majembe kutoka kwenye vyama hivi wakiyagawana na CHAUMA. Wamechukua jembe kama Mpina ambalo ni photocopy ya Magufuli kwa misimamo yake hata kwa namna anavyongea. Ana ushawishi mkubwa kwa kanda ya Ziwa na kwingineko. Kama ataungana na watu kama akina Gwajima, Warioba, Butiku, Kitwanga, Angelina Mabula nk mambo yatakuwa magumu sana kwa CCM.

CHAUMA nao wamechukua majembe yote ya chadema. Kama Freeman Mbowe na Halima Mdee nao wakaamua kujiunga na CHAUMA itakuwa fungakazi wa uwepo wa CCM. Kwani kwa mjibu wa katiba yetu inahitaji tu a simple majority kuwa raisi wa JMT.

Yaani kwa mfano ACT wazalendo kura 35% na CHAUMMA 25% tu CCM inakuwa imeshindwa hata kwani itakuwa imebakiwa na 30% ya kura assuming CUF na NCCR mageuzi watakuwa wameambulia 0%. Wizi wa kura kwenye uchaguzi huu utalindwa kitekinolojia ya security mini cameras, mawakala wasiohongeka na baati nzuri serikali imechagua balozi za nchi 12 kutoka nchi za ulaya magharibi kuwa ndiyo watakuwa waangalizi pekee wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Nchi za Afrika Mashariki na zile za SADEC zimeondolewa kuwa waangalizi.

Hivyo kwa kiasi kikubwa sana uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa huru na wazi, kitu ambacho kinaweza kuwo tishio la uhai wa chama tawala lakini wamejitakia wenyewe kwa kuyatoso baadhi ya majembe yao kama walivyofanya 2015 kwa kumtosa Lowasa.
 
Back
Top Bottom