the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Chama cha ACTwazalendo kimetoa wito kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, kusimamia maelekezo yake kuhusu rufani za wagombea ili kuhakikisha kuwa wagombea wa chama hicho waliotenguliwa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji wanarejeshwa mara moja.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu Novemba 13, 2024, inasisitiza kuwa TAMISEMI isimamie maelekezo yake kikamilifu kwani katika mchakato huo kumeshuhudiwa Wasimamizi wa Uchaguzi wakidharau maelekezo mahsusi ya kikanuni.
Soma: LGE2024 ACT Wazalendo: Kuna hujuma kubwa imepangwa dhidi ya wagombea wetu
“Ikumbukwe kuwa mnamo tarehe 09 Novemba, 2024 Kiongozi wa Chama chetu alitoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingilia kuhakikisha kuwa wagombea wa vyama vya upinzani walioenguliwa wanarejeshwa. Rai hii ilitokana na ukweli kuwa wagombea wetu walienguliwa kwa sababu za kisiasa na siyo sababu za kikanuni”, imeeleza taarifa hiyo.
Chama hicho kinasisitiza kuwa wanataka kuona hatua za haraka zinachukuliwa dhidi ya watendaji ambao wamehusika katika kuwanyima wagombea wao haki ya kushiriki kwenye uchaguzi huu kwa kuwaengua.
“Tunataka kuona hatua za kinidhamu zikichukuliwa kwa watendaji wote wa TAMISEMI waliowaengua wagombea wetu kwa uonevu na ubaguzi. Haitoshi tu wagombea kurejeshwa bali lazima kuwepo na uwajibikaji”,