Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan ameendelea kupata uungwaji mkono kutoka kwa watu mbalimbali wenye akili Timamu na wanaojitambua, pamoja na vyama mbalimbali vya kisiasa bila kujalisha itikadi zao za kisiasa.
Safari hii ACT wazalendo wameona wasiwe wanafiki na hivyo kuamua watoe na kumimina pongezi na sifa zao kwa Rais wetu mpendwa, ambapo kupitia Mjumbe wa kamati kuu ya ACT wazalendo Mheshimiwa Mansour Yussufu Himid ,ambaye mbele ya wananchi amesema ya kuwa Rais Samia ni mtu Muungwana sanaa.
Ambapo kiongozi huyo wa chama amesema ya kuwa kwa sasa hakuna watu wanaotekwa, wala hakuna watu wanao vamiwa na kufirisiwa biashara zao, wala hakuna watu au wanasiasa wanaopigwa na kutupwa ndani na wala hakuna anayezuiwa kufanya mikutano ya hadhara.
Akaendelea kusema kuwa hayo yote yanafanyika kwa kuwa kuna Muungwana katika nafasi ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.
Nami Mwashambwa Lucas najiona fahari sana na heshima kubwa sana kumuunga mkono Mama huyu na Rais wetu mpendwa aliye na moyo wa ucha Mungu, uungwana, upendo, huruma, unyenyekevu na ukarimu kwa watanzania . Kiongozi mpenda haki na mtenda haki mwenye ulimi wa hekima, busara na staha. Ndio maana huwezi kusikia akitoa maneno yenye kuwagawa au kuwaumiza watu wake.
Ni Mfariji, mlezi na Mama wa Taifa.Ni kiongozi na mama asiye na ubaguzi kwa misingi ya aina yoyote ile, wala chuki na mtu. ndio maana anawapenda watanzania wote na kuwatendea haki watu wote .ndio sababu ya Taifa kuendelea kushamiri na kutamalaki kwa umoja, upendo na mshikamano. Mungu ambariki sana Rais wetu na kumjalia Maisha marefu yenye amani, baraka na furaha.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu.