PreGE2025 ACT Wazalendo wathibitisha Sheikh Ponda kugombea Jimbo la Temeke

PreGE2025 ACT Wazalendo wathibitisha Sheikh Ponda kugombea Jimbo la Temeke

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Katibu wa Taasisi na Jumuiya za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, anatarajia kuchukuwa fomu ya kukombea ubunge na atawania nafasi hiyo katika jimbo la Temeke.

Kwa mujibu wa tangazo lililotolewa jana Juni 23, 2025 kwa umma na ACT Wazalendo, Sheikh Ponda atachukua fomu saa tano asubuhi leo Juni 24.

“Sasa ni dhahiri. Shekhe Ponda Issa Ponda kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya ACT- Wazalendo kugombea ubunge wa Jimbo la Temeke, Shekhe Ponda atachukua fomu kesho (leo) Juni 24, 2025 katika Ofisi za Chama Azimio Temeke, Muda 5:00 Asubuhi,’’ walithibitisha ACT - Wazalendo kupitia kurasa yao rasmi ya Instagram.
 
WhatsApp Image 2025-06-24 at 08.06.27_d010926e.jpg
Sheikh Ponda atachukua fomu katika eneo la Azimio Tandika Wilaya ya Temeke zilipo ofisi za Jimbo ya Chama cha ACT Wazalendo.
 
Yaani ccm waliachie jimbo la temeke kipuuzi hivi ? Huyo Ponda anajisumbua tu , bado litafungwa hata la mkono
 
CCM hatutapoteza jimbo hata 1 mwaka huu - upinzani baada ya Oktoba tukutane hapa
 
Angebaki kwenye kutetea haki za binadamu, heshima aliyoijenga kwa miaka mingi inaenda kuisha
Kwa mtazamo wako ambao sio lazima uwe sahihi.Hiyo heshima haijawai kumletea lishe zaid ya misukosuko.wacha atafute Jukwaa jingine namna nyingine yakupaza sauti yake na kujenga maisha yake.Nina amini angekua kaenda chadema usingeona heshima yake itashuka nikwasababu mmejimilikisha siasa za upinzani kituu ambacho sio sawa.
 
Sawa mkuu kila la kheri kwake
 
Back
Top Bottom