ACT Wazalendo Yaituhumu Serikali Kufeli Ahadi ya Bima ya Afya kwa Wote

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Dk Elizabeth Sanga

Chama cha ACT Wazalendo kimesema utekelezaji wa ahadi ya siku 100 ya Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Bima ya Afya kwa Wote umeshindwa kuwafikia wananchi wengi, huku kikidai kuwa watu maskini wanaendelea kukosa huduma muhimu za matibabu na vipimo vya kibingwa.

Katika tathmini yake iliyotolewa leo Agosti 27, 2026, chama hicho kimesema Serikali iliahidi ndani ya siku 100 kuzindua Bima ya Afya kwa Wote, kugharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo wenye magonjwa sugu, kuajiri wahudumu wa afya 5,000 na kukomesha kuzuiwa kwa miili ya marehemu hospitalini kutokana na madeni ya matibabu.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii wa ACT Wazalendo, Dk Elizabeth Benedict Sanga, inadai kuwa hadi sasa watu 997,015 pekee walikuwa wamesajiliwa katika Bima ya Afya kwa Wote, huku 501,981 kati yao wakiwa bado hawajapatiwa kadi.

Kwa mujibu wa chama hicho, takribani watu milioni 16.5 Tanzania Bara wanaishi chini ya mstari wa umasikini na hivyo kwa kasi iliyopo, utekelezaji wa mpango huo unaweza kuchukua takribani miaka 20 kuwafikia walengwa wakuu.

ACT Wazalendo pia imekosoa mfumo wa vifurushi vya bima, ikisema madaraja manne ya Ngorongoro Afya, Mikumi Afya, Serengeti na Tanzanite Afya yanaendeleza utofauti wa huduma kutokana na uwezo wa mwananchi wa kulipia.

Chama hicho kimesema kifurushi cha gharama ya chini kina huduma chache zaidi za kibingwa na vipimo, hali inayomaanisha kuwa wananchi wenye uwezo mkubwa wa kifedha wanapata huduma pana zaidi kuliko maskini.

Aidha, ACT Wazalendo imesema ahadi ya kugharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi maskini wenye magonjwa sugu haijatekelezwa kama ilivyoahidiwa.

Soma pia
: Rais Samia: Marufuku Hospitali kuzuia MAITI, nimeshatoa maelekezo kwa watendaji

Kwa mujibu wa tathmini hiyo, baadhi ya huduma za gharama kubwa kama uchujaji wa damu kwa wagonjwa wa figo, MRI na CT-Scan hazimo katika huduma zinazopatikana kwa walengwa maskini wanaounganishwa na mfumo huo.

Chama hicho pia kimesema bado kuna malalamiko kuhusu familia kuzuiwa kuchukua miili ya ndugu zao katika baadhi ya hospitali kabla ya kulipa madeni ya matibabu, licha ya ahadi ya Serikali kukomesha utaratibu huo ndani ya siku 100.

Katika changamoto nyingine, ACT Wazalendo imesema upatikanaji wa kadi za bima haujaambatana na uhakika wa dawa, vifaa tiba na vipimo, ikidai kuwa wananchi wenye bima bado wanalazimika kununua dawa na kulipia baadhi ya vipimo. Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa madeni ya Serikali kwa Bohari ya Dawa (MSD) yanakadiriwa kufikia Sh471.11 bilioni.

Kuhusu uhaba wa watumishi wa afya, chama hicho kimesema mahitaji ya watumishi nchini ni takribani 348,923, wakati idadi iliyopo baada ya ongezeko lililoahidiwa ni takribani 182,430, sawa na asilimia 52.3 ya mahitaji.

Kwa makadirio ya ACT Wazalendo, Serikali ingehitaji kuajiri wastani wa watumishi 33,298 kwa mwaka ndani ya miaka mitano ili kufikia mahitaji yaliyopo.

Chama hicho kimependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa Hifadhi ya Jamii kwa Wote utakaofungamanishwa na bima ya afya, ambapo wananchi wa sekta rasmi na isiyo rasmi watachangia kulingana na uwezo wao, huku Serikali ikigharamia asilimia 100 huduma kwa wananchi maskini.

Pia kimetaka kila mwanachama kupata bima moja yenye huduma sawa na inayogharamia magonjwa muhimu, pamoja na Serikali kuwekeza kwa dharura katika uzalishaji wa dawa ndani ya nchi ili kupunguza utegemezi wa dawa kutoka nje.

“Tunaamini afya ni haki ya kila mwananchi, si huduma ya anayemudu kulipia,” amesema Dk Sanga katika taarifa hiyo.
 

Sasa hivi washavurugwa, hakuna lolote la maendeleo na lenye faida kwa wananchi linalofanyika, viongozi wapo wamefura, wanapambana kwa ajili ya biashara zao, hilo liko wazi sana.
 
Kwa hiyo hii ni omission au contradiction ndugu ACT??? sasa hivi tunapiga maneno ya kimahakama tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…