Chama cha ACT Wazalendo kimeonyesha ukomavu wa kisiasa kwa kumpongeza Tundu Lissu kufuatia ushindi wake kama Mwenyekiti wa CHADEMA, nafasi ambayo pia inamfanya kuwa Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).
Kupitia ujumbe uliochapishwa na ACT Wazalendo kwenye ukurasa wao wa X (zamani Twitter), kiongozi wa chama hicho, Mwl. Macheyeki Philbert Jr, amepongeza Lissu kwa ushindi huo na kumkaribisha katika uongozi wa TCD, akiahidi ushirikiano wa dhati katika harakati za kuimarisha demokrasia nchini.