Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Abdallah Khamis, Afisa Habari, ACT Wazalendo anasema: Wakati leo Juni 05, 2025 viongozi Wakuu wa ACT Wazalendo wataongea na vyombo vya habari katika ofisi ya Makao Makuu Magomeni pia kutakuwa na tukio la Kupokea wanachama wapya wakiongozwa na Mwamba.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa rasmi kuwa mwanachama wa Chama cha ACT Wazalendo Katibu wa Shura ya Maimamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda amesema kumekuwa kukishuhudiwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ambayo vinatakiwa kupingwa.
"Tumeshuhudia raia wakitekwa (na watu wanaoitwa 'wasiojulikana) na wengine kuuliwa bila ya kupata ulinzi wa dola na utetezi wa Bunge."amesema Sheikh Ponda
Amegeza "Ndugu zangu, uzalendo unatutaka tupinge mifumo kandamizi na isiyowajibika na
kuhakikisha kuwa sheria zinalinda haki mbalimbali za wananchi."
Aidha Sheikh Ponda changamoto iliyopo nchini ni kukosekana kwa utawala wa kizalendo unaojali maslahi ya umma.
" Ndugu zangu tatizo kubwa la Nchi yetu ni kutokuwa na utawala wa kizalendo unaojali
maslahi ya umma. Watawala wet hawajali haki katika mambo mengi ya msingi na wala hawazingatii sheria" amesema Sheikh Ponda
Ambapo amedai kwamba athari za utawala wa namna hiyo ni kubwa na zinagusa kila maisha ya wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo uchumi, siasa, usalama wa raia na mambo mengine muhimu ya kijamii.