PreGE2025 ACT Wazalendo yatangaza rasmi kuwa itashiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Kupitia mitandao ya kijamii, chama cha ACT Wazalendo wamedokeza kuwa leo wana jambo lao zito ambalo wanataka kuwawasilishia wananchi.

Ni jambo gani? Fuatilia uzi huu, ujue nini kitakochoendelea kwenye mkutano huo!

View: https://www.youtube.com/watch?v=_N1YapoNlEw
WhatsApp Image 2025-04-16 at 11.16.05_bc0085e6.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kumteua kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, 2025.

=========================​

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Doroth Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu licha ya baadhi ya vyama kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo.

Doroth ameyasema hayo leo April 16 wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema wameamua kushiriki uchaguzi kuipa thamani kura za wananchi pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zimekua zikikandamiza ustawi wa demokrasia Nchini.
Dorothy.jpg
Amesema watatumia Uchaguzi Mkuu 2025 kukabiliana na watawala vyovyote vile watakavokuja lakini hawatafanya kabisa kosa la kususia.

"Tutaendelea kulinda demokrasia na tupo tayari kupambana na yoyote yule," alisema.

Pamoja na hayo kiongozi huyo wa Chama alisema wameamua kuja na maamuzi hayo baada ya kujifunza kwa kina mataifa yanayosusia uchaguzi na madhara yake.

Aidha, amesema watautumia pia uchaguzi huo kama jukwa la mapambano na kulinda demokrasia.

Pia aliongeza "Chama cha siasa ni mdau, lakini yule mwananchi ambaye yupo chini ya hicho chama analindwa kikatiba na ana haki zake za msingi. Tunafikiri baadhi ya kanuni zinavunja Katiba na tunakwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya kikatiba. Hatutaki kubaki kimya mbele ya kanuni kandamizi, lazima kuwe na rekodi kwamba tulipinga,”

Ameongeza kuwa hatua hiyo ya kisheria haiwaondoi ACT Wazalendo katika mazungumzo ya kisiasa, kwani chama hicho kinaendelea kushiriki mazungumzo kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) pamoja na makongamano mbalimbali ya kitaifa kwa lengo la kusisitiza mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi.

Katika hatua nyengine amesema Chama cha Mapunduzi CCM wameshindwa kuwatoa watanzania walio wengi kwenye dimbwi la umasikini ambao ndio kiu ya walio wengi.
 
Wakuu,

Kupitia mitandao ya kijamii, chama cha ACT Wazalendo wamedokeza kuwa leo wana jambo lao zito ambalo wanataka kuwawasilishia wananchi.

Ni jambo gani? Fuatilia uzi huu, ujue nini kitakochoendelea kwenye mkutano huo!

View: https://www.youtube.com/watch?v=_N1YapoNlEw
View attachment 3306074
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya chama chake kumteua kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba, 2025.

=========================​

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Doroth Semu amesema chama hicho kitashiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwezi oktoba mwaka huu licha ya baadhi ya vyama kutangaza kutoshiriki uchaguzi huo.

Doroth ameyasema hayo leo April 16 wakati alipokua akizungumza na waandishi wa habari mjini Unguja.

Amesema wameamua kushiriki uchaguzi kuipa thamani kura za wananchi pamoja na kuwepo kwa changamoto nyingi ambazo zimekua zikikandamiza ustawi wa demokrasia Nchini.
Amesema watatumia Uchaguzi Mkuu 2025 kukabiliana na watawala vyovyote vile watakavokuja lakini hawatafanya kabisa kosa la kususia.

"Tutaendelea kulinda demokrasia na tupo tayari kupambana na yoyote yule," alisema.

Pamoja na hayo kiongozi huyo wa Chama alisema wameamua kuja na maamuzi hayo baada ya kujifunza kwa kina mataifa yanayosusia uchaguzi na madhara yake.

Aidha, amesema watautumia pia uchaguzi huo kama jukwa la mapambano na kulinda demokrasia.

Katika hatua nyengine amesema Chama cha Mapunduzi CCM wameshindwa kuwatoa watanzania walio wengi kwenye dimbwi la umasikini ambao ndio kiu ya walio wengi.

Ahadi yetu ya kuwapa wabunge 10 iko pale pale..na tutahakikisha ACT mnakuwa chama kikuu cha upinzani na pia mtakula mema ya nchi hii.
Achaneni na hao mbumbumbu wa No reforms No Erection.
 
Kwanini ubunge utokane na ahadi na si chaguo la walio wengi kwenye uchaguzi.

Haki ni fukuto linatafuta upenyo wa kutokea, litazuiliwa ila Lina muda wake wa kulipuka.

Time will tell, doesn't matter how long it takes

Ubinafsi wetu wakula keki ya taifa sasa yasitutie upofu kutazama nchi katika vizazi vijavyo. Vizazi vyetu visijetumbukia shimo la tewa na kutulaumi sisi kama tulikuwa na akili timamu.
 
ccm inapenda vyama kama hivi visivyojitambua.....Nondo mwenyewe asimulie yaliyomkuta uchaguzi wa serikali za Mitaa 2024.....hatasahau.
 
Wafanya Biashara washapewa Chao; Kuna sababu gani ya Kutangaza? Kwa lini hawakushiriki?
 
Mimi sielewagi watu....naona wana ndimi 2....wanasema uchaguzi tangu 2019...2020...2024....kura haimui matokeo ila dola...sasa kama wameamua kuingia kwa uchaguz...means wanataka nao wapewe uongozi na dola au...maana kura haimui tena nan awe kiongozi
 
Back
Top Bottom