Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Masoud Othman Masoud ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo upande wa Zanzibar anatarajiwa kuongoza timu ya ACT katika majadiliano ya kukamilisha mageuzi ya kisheria ili kuimarisha haki, umoja na mshikamano.
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma wa ACT, Salim Bimani katika taarifa yake amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kikao cha majadiliano kilichohusisha viongozi wakuu wa chama pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ally Mwinyi tarehe 18, 2023, Ikulu ya Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo waliokutana na Rais Dkt. Mwinyi ni Zitto Kabwe ambaye ni Kiongozi wa Chama, Mwenyekiti wa Chama, Juma Duni Haji na Othman Masoud Othman ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa viongozi hao walijadiliana na kukubaliana na Rais wa Zanzibar hatua za kuchukua kukamilisha mchakato wa mageuzi ya kisheria yanayopaswa kufanyika Zanzibar ili kuimarisha Haki, Umoja na mshikamano.
Aidha, amesema viongozi wa ACT Wazalendo wamemhakikishia Rais wa Zanzibar utayari wao wa kuharakisha mazungumzo ya vyama vikuu vya kisiasa nchini Zanzibar ambayo yatasaidia utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi cha Zanzibar kuhusu mageuzi ya kisiasa, kiutawala na masuala ya Uchaguzi.
"Ili kukamilisha suala hilo viongozi tayari wamewasilisha majina ya timu ya majadiliano ya watu sita (6) kutoka ACT Wazalendo kwa Rais wa Zanzibar itakayoongozwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Ndugu Othman Masoud Othman.
“Tunataka kuhakikisha kuwa vurugu na mauaji katika chaguzi inakuwa ni jambo la historia kwa Zanzibar” alisema Kiongozi wa ACT Wazalendo Ndugu, Zitto Kabwe kuhusu mazungumzo yao na Rais wa Zanzibar.
“Tunaamini tutakubaliana kwa mambo yote ya msingi” alisema Ndugu Othman Masoud Othman kuhusu mazungumzo hayo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Ndugu Juma Duni Haji alitumia wasaa huo kumkabidhi Rais wa Zanzibar taarifa rasmi ya ACT Wazalendo kuhusu ukiukwaji wa Haki za Binaadam Zanzibar wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
"Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa ahadi yake ya kuitangaza na kuizindua Kamati hiyo wakati wowote kuanzia sasa.
"ACT Wazalendo kama taasisi inaunga mkono hatua ya viongozi wetu kukutana na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Kamati Kuu na Kamati ya Uongozi Taifa na tunaahidi kutoa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha mchakato huu unatekelezwa kwa Maslahi ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla. " ilisema taarifa hiyo ya Bimani kwa vyombo vya habari na kuongeza:
"Ni matumaini yetu kuwa kila mwenye kuitakia mema Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataunga mkono hatua hii na tunatoa wito kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza hadharani kuonesha kumuunga Mkono Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye pia nia Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.”