PreGE2025 ACT yasema imepokea Wanachama 25 kutoka CCM, Jimbo la Kojani, Wilaya ya Wete Pemba

PreGE2025 ACT yasema imepokea Wanachama 25 kutoka CCM, Jimbo la Kojani, Wilaya ya Wete Pemba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Taifa, Othman Masoud Othman amepokea Wanachama wapya 25 waliojiunga na Chama hicho kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Kojani, Wilaya ya Wete Pemba.

Vijana hao wamejiunga leo 28 Aprili 2025 katika mkutano wa hadhara unaoendelea muda huu katika viwanja vya Uwondwe Jimbo la Mtambwe.

Awali akiwakabiribisha vijana hao Mwenyekiti Mkoa wa Wete, Juma Khamis Ali amesema vijana hao wamechoshwa na madhila ya CCM ambayo wamekuwa wakifanyiwa kila siku.
WhatsApp Image 2025-04-28 at 16.54.07_3103e2b7.jpg
Amesema kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo vijana hao wataongeza nguvu ya kusimamia ushindi mkubwa wa Chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Awali vijana hao wamesema maamuzi ya kujiunga Kwao na Chama cha ACT Wazalendo yametokana na madhila mbali mbali ambao wamekua wakipitia.

Abdalla Juma Faki amesema awali waliendelea kubaki CCM wakipewa ahadi tele zikiwemo za kupewa ajira lakini hadi leo hakuna aliefanikiwa katika wao.

"Walijenga maskani kwetu Kojani wakatufanya sisi ni watu wasiojitambua lakini sasa tumeamua kuunganisha nguvu zetu pamoja kukifanya Chama cha ACT Wazalendo kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.

Maimuna Makame Issa amesema alibaki CCM akipewa ahadi tele zikiwemo za mikopo ya Serikali iliolenga kuwainua wanawake kiuchumi lakini hawana walichopewa.

"Ni bora tubaki huku na wenzetu tupambanie Nchi yetu kuendelea kubaki CCM ni kupoteza muda na nguvu kwa watu wasiojali" alisema.
 
Back
Top Bottom