Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo, Je Tuache Ushindani wa Haki Bila Haja ya Kumshindanisha na Vivuli!, ili Ada Zake Zimnenee Au...?

Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo, Je Tuache Ushindani wa Haki Bila Haja ya Kumshindanisha na Vivuli!, ili Ada Zake Zimnenee Au...?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,
Makala yangu kwenye gazeti la Nipashe la leo
Mada ya leo ni kuhusu "Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo", nikiuliza je tuache ushindani wa haki kwa wagombea wa ukweli wenye kuleta ushindani, ili tusimshindanishe na vivuli!, ili kuziacha ada za mja huyu ndizo zimnenee hiyo October, au... ni too risky kuacha ushindani wa haki, hivyo kazi ya kudhibiti matishio iendelee, kama kale kasimba ka Kizimkazi, kaendelee kufungiwa kwenye ile cage, hadi jambo letu lipite, yaani tumsimamishe mtu wetu na vivuli?
Ada ya Mja Hunena .jpg

Mimi mwenzenu, sio tuu nimepiga kura toka uchaguzi wa mwaka 1990 ambao ndio uchaguzi wa mwisho wa chama kimoja!, kwenye urais, tulikuwa tunampigia kura mgombea mmoja anayeshindana na kivuli!, Sasa tunapojiandaa kwa uchaguzi wa 2025, acheni wagombea kweli wajitokeze ili kuzuia mgombea mmoja asishindane na vivuli!.

Nimeshiriki nikiwa mwandishi wa habari na kuna wakati nilikuwa mwangalizi, na niliendelea kushiriki chaguzi zote za vyama vingi, toka ule uchaguzi mdogo wa jimbo la Kwahani, 1994, uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, 2000, 2005, 2010, 2015, 2020, na sasa 2025, hivyo kuna vitu niliviona naweza kuvitolea ushauri wa busara, kwa kuviandika, vinaweza kusaidia jambo kuelekea uchaguzi wa 2025 huku nikiwafunza vijana wa leo, busara zilizomo ndani ya ngano za lugha yetu adhimu ya Kiswahili. Wakati wetu tulifundishwa hadithi, methali, vitendawili, nahau, na tamathali za semi.

Mada ya leo ni ya tamathali za semi hii ya Kiswahili isemayo "Ada ya Mja Hunena, Muungwana ni Kitendo“, ni sawa na ile semi inayosema "Matendo hukidhi haja maridhawa kuliko maneno"

Ada ya mja hunena, ada ni matendo, mja ni mtu, kiumbe wa Mwenyeezi Mungu, Ada ya mja hunena, ni matendo ya mtu anayotenda yananena, yana sauti, yana msemea, badala ya mtu kusema kwa maneno, nimefanya hiki au nimefanya kile, wewe tenda, fanya kitu cha kuonekanikani, halafu matokeo ya matendo yako, au matokeo ya ulichokifanya ndio yakusemee!, ukifanya jambo jema zuri la kuonekanika, huna haja ya kusema, umefanya nini, acha watu waone kilichofanyika, halafu hicho kilichofanyika ndio kinakuenea. Neno muungwana ni kitendo sio kauli au maneno "mimi muungwana", tenda uungwana, halafu hayo matendo yako ya uungwana au kiungwana ndio yakunenea na kukusemea, fulani ni muungwana!.

Binadamu siku zote, huwa hawana mema, sio watu wote ni watu wema, kuna wengine ni mahasisidi, hasidi huwa hana sababu!, kuna watu sio wana wema, hata uwatendee mema makubwa kiasi gani, ipo siku, watakutenda tuu!, ndio maana. Waswahili wanamsemo wa "Tenda wema uende zako, usisubirie shukrani", na mahali penye wema, kuna msemo, “pema usijapo pema, ukipema, sii pema tena”, ukitenda jambo jema, usijisifu kwa jema hilo, ukijisifu, hilo jema litatafutiwa ubaya!.

Nimeleta mada hii baada ya kuangalia mubashara kupitia TBC, uzinduzi wa daraja la JPM, Kigongo - Busisi, nikakumbuka daraja la Tanzanite, nikakumbuka flyover ya Tazara, Interchange ya Ubungo, Mradi wa JNHPP, nikakumbuka reli ya SGR, serikali kuhamia Dodoma, Ikulu ya Chamwino, mashule, mahospitali, mabarabara kibao, midege ya ATCL tulioinunua kwa kupiga tanchi!, na maendeleo mengine mengi makubwa ya kuonekanika, nikajisemea kimoyo moyo, “kiukweli Yule Kaka yangu, alikuwa na uthubutu mkubwa!, kuna baadhi aliyatekeleza wala hayakuwemo kwenye ilani, ila pia kuna yaliyokuwemo kwenye ilani, akaachana nayo kwasababu sio kipaumbele chake.

Pamoja na wema wote huo, ulipofika muda wa kutwaliwa, Kaka alitwaliwa na Dada akaingia na kukamilisha yale mema makubwa mazuri ya kuonekanika anayoyatenda mja huyu aliyepo sasa, kwanza kwa kukamilisha yale ya mtangulizi wake, kisha kujumlisha na ya kwake anayotenda, kiukweli kabisa, matendo yake yamekidhi haja maridhawa kuiko maneno!, hivyo Watanzania tuwe waungwana, anastahili kushukuriwa kwa kupewa shukrani ya asante stahiki!.

Kitendo cha mtu kufanyiwa wema mkubwa hivi, halafu kuwa mtovu wa fadhila, kuwa mtovu wa shukrani, kutomshukuru mtu kama huyu ni kujichumia tuu bure ile dhambi! ya utovu wa fadhila na utovu wa shukrani!

Watanzania walio wengi ni waungwana sana, ni wastaarabu sana, na ni watu wa shukrani na kukumbuka fadhila, sio watovu wa shukrani kivile!, hivyo utakapo wadia ule muda wa kutoa shukrani, Watanzania watampatia shukrani zake stahiki!.

Wakati wote, mema haya, makubwa na mazuri haya yakiendelea, kuna walevi, wamelewa na wanaiga kelele sana kuwa hakuna chochote kilichofanyika!, kuna msemo mwingine wa Kiswahili, unaitwa "kumsukuma mlevi". Unamuona mlevi amelewa chakari, anatembea kwa kuyumba yumba, yaani ni amelewa tilalila!, ukimsukuma kidogo tuu, ni anakwenda chini, na jinsi pombe zilivyomzidia, akienda chini, anaweza hata kudondoka mtaroni, akashindwa kuinuka ikawa ndio mtolee!, mtu ameondoka jumla!.

Kufuatia shukrani za Watanzania kwa mja huyu, kwa kilichofanyika, hakuna kabisa sababu ya kumsukuma huyu mlevi, mja wetu, usimsukume kabisa, huyu mlevi, mwache aendelee kutembea kwa kupepesuka na pombe zake, atajiangukia mwenyewe, bora lawama za kutomsaidia mlevi kwa kumwacha akapepesuka hadi akaanguka mwenyewe, kuliko fedheha ya kumsukuma mlevi akaanguka, na ile anguka yake ikawa ni ile anguka ya mtolee!. Lawama utabebeshwa wewe kwa kumsukuma!.

Asante stahiki kwa huyu mja aliyepo ni ile asante ya ile siku ya siku, ni unachukua, unaweka, !, ..

Hivyo namshauri aliyepo, awape tuu kila wanachokitaka, hata kama hawastahili, ali mradi, wameomba, wanapiga makelele sana, yanatukosesha usingizi, wapewe tuu!

Wasipopewa, baada ya Watanzania kuonyesha shukrani zao kwa yaliyofanyika, mtakuwa mmewapa uhalali wa lile jambo letu lile, watasema yule aliyepita sio amepita kwasababu alistahili, watadai ni amepita kwasababu, amesimama na vivuli, mshindani wa ukweli, amefanyiwa figisu ya kubambikiwa kesi mbaya ili kuhalalisha kumhifadhi pahala salama kupisha jambo letu, hivyo aliyeshinda, ameshinda kwasababu ameshindanishwa na kivuli, au vivuli!.

Naendelea kushauri, kale ka simba ka Kizimkazi, kaondolewe tuu kwenye ile cage, katatusumbua sana kwa kupigiwa kelele kutoka karibu kila kona!.

Hebu tuwape tuu wanachotaka, tuingie uwanjani kwenye uwanja ulio sawa, ( a level playing field), tuboreshe kanuni za mchezo kwa fair play, tuweke refa mtenda haki, mwisho wa mchezo, mshindi apatikane kwa haki, tufurahie ushindi wa haki, tena kwa hisia zangu, hizi mambo za figisu, zinaweza kuwa ndio zimechagia kwenye ile karma iliyopelelekea lile tukio lile kutokea!, tusipojirekebisha hii 2025, tukio kama lile linaweza kuja kujirudia!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Kama CCM ni chama kikubwa mbona kinaogopa katiba mpya,kinaogopa mabadiliko ya tume,kinaogopa watu kukosoa,kinauwa na kuteka watu kila uchwao ,kimefika mahali kinaenda hadi Kwa maaskofu wa makanisa 😭 ,yaani hii Ndio Sera ya TANU?Mayalla kizazi kijacho kitaweza kuandika haya makala kama za kwako kama huko vyuoni saizi hakuna mijadala ?Vyuoni vimekuwa kama shule za msingi ,kama chama hizi Sera mnazoandaa Nani atachambua kama hamtaki raia wazungumze!Mayalla inawezekana hata hapa nyumbani kwako watoto wako umewangia ndani wasiongee na majirani😭 mumefikia mbaliiiiii zaidi mnageuza watu kinyume na maumbile .Pascal Mayalla mwisho nikuambie Ndugu zako wamesombwa Kwa malori mikoa mitatu Shinyanga,Tabora,Geita,na Mwanza
 
Easy tu, futeni sheria ya vyama vingi mbaki wenyewe tu, mbona tuliishi tu kabla ya hapo? Kwa nini mnateseka na mlileta sheria wenyewe na mna uwezo wa kupeleka kwenye kikundi cha chawa wa jiwe pale Dodoma watagonga meza tu ili mama ashindane na kivuli chake na sisi kenge tufanye mengine tu ya kutafuta rizki za vifaranga wetu, mle nyie tu!
 
No reforms no election
Tumechoka kuibiwa kura.
Kwa hivyo kama mmechoka kuibiwa kura, hiyo NRNE itazuiaje wizi wa kura?.

Ili kulinda kura, kitu cha kwanza ni kujitambua na kuiyambua thamani ya kura yako,
Kitu cha pili ni kujua kura zinaibiwaje?

Ndipo uweze kulinda kura.

Ili wizi wa kura utokee ni lazima kuwepo watu waliojiandikisha lakini hawajitokezi kupiga kura, hivyo zile.kura zao ambazo hazikupigwa, zinapigwa tiki na kumpa mgombea wao!.

Kama watu wote.mtajiandikisha kupiga kura na siku ya uchaguzi wote mtajitokeza kupiga kura, kutakuwa hakuna kura za kuiba!
Hiyo NRNE ingekuwa na maana kama ingekuwa NRVO yaani bila reforms, piga chini, ingewahamasisha kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari na siku ya uchaguzi kujitokeza kwa wingi to vote out, hivyo upinzani kuchukua nchi!

Thamani ya Kura Yako: Je Wajua Wewe Ndiye Mwajiri wa Rais wa JMT kwa Kura Yako na Kumlipa Mshahara Wake Yeye na Serikali Yake Yote kwa Kodi Yako?.
P
 
Kwa hivyo kama mmechoka kuibiwa kura, hiyo NRNE itazuiaje wizi wa kura?.
P
Wakisema NO REFORMS NO ELECTION huwa unaelewa lakini?
Unawajua maafisa uchaguzi huko halmashauri ni akina nani?
Wale walimu wanaosimamia uchaguzi unajua kazi zao?
DEDs no kina nani unajua?
Pascal kuwa mwandishi wa siku nyingi hakumaaishi kuwa unajua kila kitu
 
Wakili msomi ccm ni waoga sana na hawataki kusikia faiir ground. Kwa kazi aliyoipiga mkuu ya kumalizia miradi mikubwa kama JNhPp. Kigongo busisi. Sgr. Irrigation systems and watee. Yaani kwenye box la.kura atashinda kwa kishindo.
Ila kuna watu project zao ni kuzua hekaheka ili wapate pesa ndio wanajaza upepo yule simba wa kizimkazi afungiwe.
 
Wanabodi,

Kitendo cha mtu kufanyiwa wema mkubwa hivi, halafu kuwa mtovu wa fadhila, kuwa mtovu wa shukrani, kutomshukuru mtu kama huyu ni kujichumia tuu bure ile dhambi! ya utovu wa fadhila na utovu wa shukrani!

Watanzania walio wengi ni waungwana sana, ni wastaarabu sana, na ni watu wa shukrani na kukumbuka fadhila, sio watovu wa shukrani kivile!, hivyo utakapo wadia ule muda wa kutoa shukrani, Watanzania watampatia shukrani zake stahiki!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Ni katika kukumbushana tuu, with 7 days to go kabla ya Uchaguzi, nawakumbusha tuu niliwahi kiandika nini humu kumhusu Rais Samia Suluhu Hassan, na uwezo wake wa urais wa JMT.

Hiyo October 29 tukiamua kumpa tena mitano mingine, then atafanya better and better!
Tumpe!.

Paskali.
 
Back
Top Bottom