Ada za shule na michango yake

Gwaje

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
299
Reaction score
85
Imekuwa ni utaratibu uliozoeleka sasa Tanzania kwa shule nyingi ikiwamo pamoja na za Serikali na hata za watu binafsi pia hata Vyuo mbalimbali kuwa na tozo mbili za huduma.

Kazi au biashara kubwa ya shule au chuo ni kufundisha wanafunzi, na ili kumfundisha kijana huyu zipo gharama sina tatizo na hizo gharama. Tatizo lipo kwenye makundi ya gharama wakati wewe ndiye uliyepanga na pia ndiye mtumiaji je mantiki yake hasa huwa nini.

Shule au chuo kinasema ada yetu tsh 1000000, Michango 200000 ambapo michango hiyo hairudishwi kama haitatumika yote sasa sijui huu ni wizi au kiini macho.

Mtazamo wangu shule na vyuo vingesema ada Tsh1200000 basi badala ya kuongeza vigharama kila muhula kwa lugha ya wizi iitwayo michango ya chuo au shule.
 
Shule za kata zina michango michache tu;

Ada _20000, Taaluma_10000, Mlinzi_20000, mpishi_10000, chakula mchana_80000, dawati_50000, afya_10000, michezo_10000, necta F IV_50000, kitambulisho 5000, graduation_20000, ukarabati_10000

Nikikumbuka mingine nitawaandikia! Hii ni baadhi tu...
 
1. kulipia mlinzi

2. wino wa kuchapa mitihani

3. fagio na madekio

4. karatasi za mitihani

5. dharura

Sasa haya c sehem ya ada ulolipa ktk mambo ya shule kwa nn tunachangishwa separate ?
 
Gwaje

Serikali ilisema imefuta ada ya Sh 2,000/= shule za msingi. Sasa michango na uandikishwaji ni zaidi ya Sh 30,000/= ndipo mtoto asome. Hata hiyo gia ya kusema inafuta ada sekondari ni uongo. Hiyo ni sawa na kusema inapandisha ada ila itatumia jina MICHANGO.

Subiri uone au waulize wanaosomesha shule za misingi kuwa nafuu ilikuwa wakati gani kati ya sasa na wakati wa ada ya Sh 2,000/=
 
Last edited by a moderator:
Shida no kwa mlaji maana nchi hii mpishi ndiye mwamuzi mwanzo mwisho. Nadhani IPO siku tutafanya maamuzi sahihi
 
Ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga.
 
Ukiona elimu ni gharama jaribu ujinga.

na wew ulipata za escrow? unavosema ukiona elim ni garama jarib ujinga wew ni wale wale walaj wa hela za watanzania
kwa nch yenye kila maligaf kama hi ilibid kusoma kwa sh 0/= za kitz tuwe makn tunaendeshwa mno!
 
na wew ulipata za escrow? unavosema ukiona elim ni garama jarib ujinga wew ni wale wale walaj wa hela za watanzania
kwa nch yenye kila maligaf kama hi ilibid kusoma kwa sh 0/= za kitz tuwe makn tunaendeshwa mno!

Usiogope kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake.
 
yaaani ni shida michango chungu nzima, shule za kata huku watoto wanapigwa vibaya , sijui kwa sheria gani!! walimu hawatambui wanachostahili kufanya!! mtoto analazimishwa kutoa ada na michango kwa fimbo utadhani kajizaa mwenyewe. hasa walimu vijana hao wenye degree feki hata kufundisha hawawezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…