Amani Msumari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,833
- 979
Mbenge,Mkuu, kuna kauli na misemo ya kichama imetolewa mara kwa mara mpaka sasa imeshachosha kusikika tena masikioni mwa Watanzania. Kuiweka awamu hii kama alama yenye kukumbukwa ktk mapambano dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu na rushwa itakuwa ni kitu cha ajabu mno.
Wana CCM Wana kwa mbwembwe wanajisifu kwa ujenzi wa miundombinu na kuongezeka kwa huduma za afya na elimu, lkn wanasahau jambo moja muhimu kuwa hayo yote hufanyika kwa kupitia kodi na maduhuli mengine yalipwayo katika fuko la hazina, vilevile na mzigo wa madeni makubwa ambao wanatubebesha Watanzania wote yakifanyika kwa usiri mkubwa.
CCM kama chama tawala pekee hapa toka wakati wa uhuru, kimepewa ridhaa ya kuiongoza serikali, hivyo kupata uhalali wa kumiliki fuko la hazina. Kwa hiyo hizo kauli za sijui kujibadilisha, sijui tumeweza kutekeleza, na upuuzi mwingine kama huo zinakerehesha sana.
Ni kutaka kutafuta kiki ili kujipa "ownership" kwa vitu ambayo kimsingi ni vya kawaida kufanywa na serikali yoyote ile duniani. Hzo kauli ndizo huwafanya wana CCM kuwa wavivu ktk kufikiri na hata kuona mambo mengine mazuri nje ya kasha la fikra pana na maono sahihi kwa mustakabali wa Taifa letu.
Tuingie kazini kuleta ushindi mkubwa kwaajili ya mambo makubwaSawa
Unajidanganya weweMbenge,
Kila mtu ashinde mechu zake na mtu hahukumiwi kwa dhambi ya baba yake.
Kuihukumu serikali ya awamu ya tano kwa ishu za awamu ni kutaka kupoka haki ya serikali hii ambapo watanzania hilo wamelikataa.
Kuhusu Kodi elewa kuwa hata Sudani ya kusini na Somalia pia wanakusanya Kodi. Ishu hapa ni matumizu sahihi ya kodi hiyo
CCM chini ya Rais Magufuli imefanya kwa vitendo. Ndugu yangu, kura yako ni ya thamani sana, kura yako mpe John, mpe mbunge na diwani wa CCM kwasababu mwaka huu tumewaletea kile kilicho bora kabisa, ile kitu roho inasuhuzika
Wewe wasema
Washiriki kwenye kukipatia chama ushindiKweli ni kikosi cha maangamizi. Waliokatwa watulie waache tamaaaaa
Chama kikongweChama chakavu na wapiga zumari wasiojielewa...
Amani,Mbenge,
Kila mtu ashinde mechu zake na mtu hahukumiwi kwa dhambi ya baba yake.
Kuihukumu serikali ya awamu ya tano kwa ishu za awamu ni kutaka kupoka haki ya serikali hii ambapo watanzania hilo wamelikataa.
Kuhusu Kodi elewa kuwa hata Sudani ya kusini na Somalia pia wanakusanya Kodi. Ishu hapa ni matumizu sahihi ya kodi hiyo
CCM chini ya Rais Magufuli imefanya kwa vitendo. Ndugu yangu, kura yako ni ya thamani sana, kura yako mpe John, mpe mbunge na diwani wa CCM kwasababu mwaka huu tumewaletea kile kilicho bora kabisa, ile kitu roho inasuhuzika
Sawa. Hayo yote unayoyataja, mgombea wetu anayoAmani,
Suala la uthamani wa kura yangu nalitambua sana, ndiyo maana nataka kwanza kusikiliza sera za vyama vilivyopo ktk kinyang'anyiro na pia kupima umakini na uthabiti wa hoja wa wagombea mbalimbali ambao wameaminiwa kuzipeperusha bendera za vyama vyao.
Jukumu langu ni kuwapima, kuwachuja na hatimaye kujridhisha kuwa nani hasa ambaye nipaswa kumtendea haki kwa kumpa kura yangu. Kwa nafasi ya uraisi nitazingatia ubora wa kunadi sera zao bali kwa mbunge na diwani nitaangalia wasifu wao wa utendaji kwa kwa nafasi ambazo walikwisha wahi kuzitumikia.
Rais ni mtu ambaye anaweka matumaini ya kesho ya Watanzania kupitia kuitii, kuitunza na kuilinda katiba ya nchi yetu, sheria, kanuni na taratibu zake kama vile zinavyoainishwa. Sitegemei kumsikia mgombea wa nafasi ya urais akijinadi kwa kutaja majukumu yake ya kila siku kama ndiyo "benchmark" ya mafanikio yake.
Zaidi tunatarajia kuwasikia wakinadi sera za kuleta mageuzi makubwa ya kijamii na kiuchumi na huku wakijipambanua kwa kudumisha umoja wa Taifa letu. Watanzania wanahitaji haki wala siyo utulivu ambao umefichwa ndani ya neno "AMANI"
Hoja ni ipi hapo?kweli magu kafanya makubwa 😁😁