Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Levis Gervas Mahenge mkazi wa Ngiu Halmashauri ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe ameiomba serikali kuingilia kati ili kupata matibabu kutokana na majeraha pamoja na kuvunjika kwa mkono baada ya kudaiwa kupigwa na mkuu wa kituo cha Polisi Makete Mjini kilichopo wilaya ya Makete kwa madai ya kutoa lugha chafu mtaani dhidi ya mkuu wa kituo, tukio ambalo amelihusisha pia na kuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke ambaye ameelezwa kufahamiana na mkuu huyo wa kituo.
Akizungumza na Jambo TV, Mahenge amesema licha ya maumivu anayoyapata lakini mpaka sasa hakuna msaada anaoupata kutoka kwa mkuu wa kituo huku akiwa ametelekezwa na kupata tabu dhidi ya majeraha aliyonayo.
Fedrick Gervas Mahenge ambaye ni kaka wa Levis Mahenge ameeleza juu ya sakata la mdogo wake ambapo amebainisha maamuzi ya Mkuu wa Wilaya ya Makete ni kuwa mkuu wa kituo anapaswa kugharamia matibabu, malazi mpaka chakula kwa mgonjwa mpaka atakapopona ndipo akabidhiwe kwa ndugu lakini wanashangaa kuona hakuna jambo linalofanyika.
Jambo TV pia imezungumza na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Mahamoud Hassan Banga ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akibainisha kuwa uchunguzi wa tukio unaendelea na taarifa rasmi itatolewa kwa umma pale uchunguzi huo utakapokamilika.
Kupata undani wa taarifa hii na mkasa mzima, tembelea chaneli yetu ya Youtube ya JAMBO TV.