chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mwanza imepoteza kiongozi mwana maendeleo, amehamishwa kuelekea Mkoa wa Morogoro.
Adam Malima hakika aliifuatilia miradi ya maendeleo kwa moyo mmoja, na hakusita kuwabana watu waliokuwa wanatapanya Mali za Wana mwanza.
Ujenzi wa uwanja wa ndege aliufuatilia Kila siku, pale mwanza jengo la abiria lilijengwa kama stoo ya kuhifadhia pamba au tumbaku, amepambana mpaka ramani imerekebishwa, amepambana mpaka ujenzi inasimamiwa na mamlaka ya viwanja vya ndege kutoka manispaa, piga picha uwanja ulijengwa na manispaa! Upigaji kushoto kulia, mchoraji wa ramani ni fundi mchundo tu.
Daraja la busisi alisimamia Kila siku ya Mungu, mwakani linaisha.
SGR alikuwa nao mguu kwa mguu, kaiacha imesonga mbele.
Mambo kede kede.
Sijui kwa nini kahamishwa, lakini kwa hakika mwanza iliridhika na kutulia chini ya uongozi wake, na bado inamuhitaji sana, walau kwa miaka mitano zaidi alistahili kuwa pale.