Adam Malima, kiongozi aliyependa maendeleo ya Mkoa wa Mwanza, hakika utakumbukwa

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Mwanza imepoteza kiongozi mwana maendeleo, amehamishwa kuelekea Mkoa wa Morogoro.

Adam Malima hakika aliifuatilia miradi ya maendeleo kwa moyo mmoja, na hakusita kuwabana watu waliokuwa wanatapanya Mali za Wana mwanza.

Ujenzi wa uwanja wa ndege aliufuatilia Kila siku, pale mwanza jengo la abiria lilijengwa kama stoo ya kuhifadhia pamba au tumbaku, amepambana mpaka ramani imerekebishwa, amepambana mpaka ujenzi inasimamiwa na mamlaka ya viwanja vya ndege kutoka manispaa, piga picha uwanja ulijengwa na manispaa! Upigaji kushoto kulia, mchoraji wa ramani ni fundi mchundo tu.

Daraja la busisi alisimamia Kila siku ya Mungu, mwakani linaisha.

SGR alikuwa nao mguu kwa mguu, kaiacha imesonga mbele.

Mambo kede kede.

Sijui kwa nini kahamishwa, lakini kwa hakika mwanza iliridhika na kutulia chini ya uongozi wake, na bado inamuhitaji sana, walau kwa miaka mitano zaidi alistahili kuwa pale.
 
Mwanza huwa inasalitiwa na kuhujumiwa kwa kila aina lakini bado inasonga mbele tu. Sasa hivi imepelekewa huyu mlevi mwana siasa.
Kwa sasa RC wa Mwanza ni nani baada ya kuhamishwa kwa ustadh Adam Kighoma Ali Malima?
 
Morogoro ndiyo mkoa pekee ambao mimi naamini unakua kwa kasi bila ya mbeleko ya Serikali. Ni mkoa wenye natural resources nyingi.
 
🤣🤣🤣malima umetuma katibu wako aje akupigie pande,baada ya kuona chalamila na makala wametake headlines🙏 Hatudanganyiki 🏂
 
Adam Malima amefanya kazi nzuri Mwanza muda mfupi kwenye miradi, sijui makala atawezaje, wacha tuone. Mwanza ina bahati mbaya Daniel Njolay aliwahi kukaa miezi 6 tu Mwanza akaibadilisha akahamishwa Mwanza kwenda Rukwa, Mza ikapotea kabisa kuanzia hapo. Huyu naye Malima kachomolowa chap chap pamoja na kelele zake kuhusu uwanja wa ndege, daraja nk. Mza kwishney
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…