Adam Nditi yuko wapi?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Huyu ni kijana wa Tanzania aliyekuwa anakipiga Klabu ya Chelsea ya watoto, lakini ghafla akaja akatemwa na klabu hiyo, baada ya hapo sijui alikwenda wapi, mnaojua alipo mtanzania huyu ambaye tuliaminishwa kuwa ana kipaji cha hali ya juu, njooni mtujuze alipo sasa
 
Usishangae kusikia yupo Nungwi ya Zanzibar!!!
Ngoja wadau waje wadadavue.
 
Dogo 'alifuata' ushauri wa watu kama kina shaffih wakampoteza, kama alikuwa ma lengo la kuendelea kimpira angekubali kuchezea stars, aliadanganywaga ana nafasi kukipiga the 3 lions, akagoma stars! Pia alijikita sana kwenye kupata uraia wa Uk zaidi ya soka! Ndo kumempoteza.
 
Shaffih anaingiaje
 
Anacheza non league teams huko, sijui kama atarudi kwenye form
 
Kwa maono yangu ni kwamba dogo hajachelewa, kwa CV aliyonayo anaweza kuja kujaribu bahati hata league zinazolipa vizuri Africa eg. League ya south Africa au Egypt na nchi nyingine za kaskazini mwa Africa. anaweza kupata timu itakayomlipa vizuri na akaanzia hapo kusogea you never know may be baada ya miaka miwili au mitatu kama ata-focus kwenye ku-improve game yake anweza akaonekana na timu nyingi za ulaya akapita njia anayopita samatta sasa hivi may be by the time akiwa na 24 au 25 akawa kafika kwenye level aliyoitarajia akiwa Chelsea.

Huwa naamini sana kwenye exposure kwa wachezaji na dogo kwa sababu amepita kwenye academy kubwa kam ya Chelsea uwezekano wa yeye kupenya kirahisi ni mkubwa kuliko wachezaji wengi wanaopita kwenye mifumo yetu ya kimpira huku Africa.....na kingine nnachoweza kumshauri ni kuwa asahahau suala la kucheza three lions arudi tu acheze taifa stars naamini kwa kucheza nation team itamuongezea credits na inaweza kumfanya kuonekana kirahisi.

muda bado unaruhusu dogo kufika alipotarajia, naamini akiamua ataweza njoo uanze huku uwaprove wrong wote wanoamini umepotea..........mafunzo yako hapo Chelsea academy hayawezi kwenda hivi pigania malengo yako na rudi ucheze nation team ya nyumbani coz muunganiko wako na watu kama kina samatta unaweza kutusogeza atleast 2019 tukacheza hata AFCON kama wenzetu Uganda.
 

Mkuu, huyu dogo anachezea timu moja ndogo ya mji mmoja unaitwa Guilford nchini Uingereza.

Aliondoka Chelsea baada ya kuwa nyuma kwenye uchaguzi au "pecking order".

Pale Chelsea pana ushindani sana na ukizingatia katika nafasi aliyoizoea Adam ya beki wa kushoto, tayari kuna vijana wenzie kama Ryan Bertrand na Patrick van Aanholt ambao pia wanachezea nafasi hiyo.

Kama ilivyo kwa wachezaji wengine Adam alikuwa na mkataba na Chelsea lakini ameamua kuachana na timu hiyo kubwa na kwenda kucheza ligi daraja la pili.

Sijaelewa mantiki ya Adam kuchukua uamuzi huo kwasababu Charles Musonda (kiungo wa zamani wa Zambia) ana watoto wake watatu wapo Chelsea Charly na kaka zake Tika na Lamisha na wanacheza vizuri tu zikiwemo mechi kama Ligi kuu ya watoto under 21, FA youth Cup na ligi ya vijana ya UEFA.

Hawa watoto wamezaliwa Ubelgiji lakini wameanzia kuchezea mpira kwenye kitalu cha timu ya Anderlecht na Charly sasa hivi anachezea Real Betis ya Spain kwa mkopo.

Labda historia inamsumbua Adam Nditi au anajiona yeye ni star na amemaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…