Adeyun Saleh na Paul Godfrey wawaachie nafasi Edward Manyama na Shaban Djuma

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Licha ya kuwa Yanga haijapata kupoteza mchezo wa kiushindani msimu huu wa 2020/21, bado kuna haja na sababu ya kuhakikisha tunaimarisha safu ya ulinzi ili kuhakikisha tunapunguza idadi ya magoli ya hovyo hovyo tunayo fungwa.

Katika eneo pekee la ulinzi ambako kuna shida ni eneo la mabeki wa pembeni.

Kwa kipindi kirefu kumekuwa hakuna wachezaji wenye kaliba ya kufanana kiuwezo. Wachezaji waliopo ni wakawaida sana. Na hata kukosa hadhi ya kumwezesha mwalimu kufanya rotation ya wachezaji kutokana na uwezo wao.

Katika dirisha la usajili la msimu ujao ni vyema kufanyike kwa ongezeko la wachezaji kama Edward Manyama (ruvu) na Shaban Djuma (vita). Wachezaji kama Adeyun Saleh na Paul Godfrey inabidi wakatafute changamoto pahala pengine. Tunataka kuongeza ushindani katika eneo la ulinzi ili kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa msimu ujao wa 2021/22.

Ni wakati wa kuirudisha team katika Ubora wake sasa.
 
Haya sasa ndo mawazo yanayotakiwa....Yaani kuimarisha Timu kwa msimu UJAO....Lakini utamuona mtu kakaza shingo kuongelea Ubingwa msimu huu ni kama kujisumbua. Mnyama Simba anakuja wanguwangu, bora kupanga mikakati miaka ijayo! Timu Yenyewe Ya Ubingwa IPO WAPI?
 
Mkuu unaota ndoto gani hivi umefatilia mahojiano ya Shungu, pamoja na kuwa kocha wenu anasema anaifatilia sana Simba kutokana na aina ya wachezaji ilionao na aina ya mpira wanaocheza hivi kama mnashindwa kumlipa Tambwe huyo ndio mtamuweza
 
Licha ya kuwa Yanga haijapata kupoteza mchezo wa kiushindani msimu huu wa 2020/21, bado kuna haja na sababu ya kuhakikisha tunaimarisha safu ya ulinzi ili kuhakikisha tunapunguza idadi ya magoli ya hovyo hovyo tunayo fungwa.

Katika eneo pekee la ulinzi ambako kuna shida ni eneo la mabeki wa pembeni.

Kwa kipindi kirefu kumekuwa hakuna wachezaji wenye kaliba ya kufanana kiuwezo. Wachezaji waliopo ni wakawaida sana. Na hata kukosa hadhi ya kumwezesha mwalimu kufanya rotation ya wachezaji kutokana na uwezo wao.

Katika dirisha la usajili la msimu ujao ni vyema kufanyike kwa ongezeko la wachezaji kama Edward Manyama (ruvu) na Shaban Djuma (vita). Wachezaji kama Adeyun Saleh na Paul Godfrey inabidi wakatafute changamoto pahala pengine. Tunataka kuongeza ushindani katika eneo la ulinzi ili kupunguza idadi ya magoli ya kufungwa msimu ujao wa 2021/22.

Ni wakati wa kuirudisha team katika Ubora wake sasa.
Huyo Djuma....MlTAKO MBWATAMBWATA FC watakuwa wameshamuwahi ili mradi tu asije kwa WANANCHI...
 
Ana mkataba na AS Vita mpaka 2023. Kama mkataba ungekuwa umevunjwa kwa kitika cha pesa basi habari ingekuwa imeenea sana.
 
Back
Top Bottom