Na hii ipo Dar, kuna ngapi kama hizi zipo Ludewa, Tunduru, Kakola, Rwamisheni, na pengine popote..???ADHA HII ITAISHA LINI! Wednesday, 21 October 2009 08:02
Wanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Vingunguti katika Manispaa ya Ilala, Dar es salaam wakifanya mitihani ya "mock" wakiwa wameketi sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati unaoikabili shule hiyo. (Picha na Gladness Theonest)
Nilienda Kilindi na Mkinga wilaya za Mkoani Tanga kuna matatizo kama haya tena makubwa saana. Si kukaa chini tu bali hakuna madarasa kabisa hata ya wanafunzi kukaa na kusoma. Wakati wa mvua wanaondoka na kurudi nyumbani hakuna shule siku hiyo na kipindi chote cha masika. Just imagine halafu tunakaa tunajidanganya kuwa hii nchi kuna amani na usawa wakati rasilimali za muhimu hazigawanywi sawasawa miongoni mwetu. Ni tatizo halafu bado serikali inakaa na kusema imeongeza idadi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za msingi na sekondari. LOL!🙁Na hii ipo Dar, kuna ngapi kama hizi zipo Ludewa, Tunduru, Kakola, Rwamisheni, na pengine popote..???
Adha hii imeanza baada ya jamaa wa mikoani kukimbilia bongo... Bongo imejaa!Kwani hii adha imeanza lini? Ukipata jibu lake ndo unaweza kukisia itaisha lini....
Adha hii imeanza baada ya jamaa wa mikoani kukimbilia bongo... Bongo imejaa!
ADHA HII ITAISHA LINI! http://majira.co.tz/index.php?view=...bali&id=1731:adha-hii-itaisha-lini&format=pdf http://majira.co.tz/index.php?view=...hii-itaisha-lini&tmpl=component&print=1&page= http://majira.co.tz/index.php?optio...pY2xlJmlkPTE3MzE6YWRoYS1oaWktaXRhaXNoYS1saW5p Wednesday, 21 October 2009 08:02
Wanafunzi wa Darasa la Nne katika Shule ya Msingi Mtakuja iliyoko Vingunguti katika Manispaa ya Ilala, Dar es salaam wakifanya mitihani ya "mock" wakiwa wameketi sakafuni kutokana na ukosefu wa madawati unaoikabili shule hiyo. (Picha na Gladness Theonest)
Kwa hiyo hii adha iko "bongo" tu na mikoani haipo?
Katika hili ni vema kujua jamii hiyo ina viupa mbele vipi? Pengine hilo la kukaa chini sio kero kwao. Kwani sehemu nyingine wazazi na wafanyabiashara wamekuwa wakisaidiana na serikali zao za mitaa kuondoa tatizo la madawati.Hapa tuache kulaumu serikali tu. Hili ni tatizo la jamii nzima. Sasa cha kujiuliza jamii inafanya nini? Kwa nini watu hatu step up to the plate kubadilisha hizi hali? Kwani wazazi wa watoto hao na watu wengine wapenda maendeleo wakikusanya nguvu zao watashindwa kweli kuchongesha madawati au kununua viti vya kukalia hao watoto?
I'm tired of people boohooing govt this govt that....why don't we all step up as a community?