Millionea
Member
- Oct 9, 2012
- 58
- 18
Maswali ninayojiuliza katika sakata hili la kuongezeka kwa nauli ni mengi. Na mengine ni mazalia ya machungu ya adha na taabu wanazopata wanafunzi kwenye daladala.
Hoja yangu ni Je haki za wanafunzi zitaheshimiwa nauli ikipanda? Huduma kwa wanafunzi itaboreshwa nauli ikipanda? Na lini tatizo la wanafunzi litakwisha kabisa? Nani anawajibu wa kusimamia usafiri huu?
Nadhani, wanafunzi kulipa Sh 200 kwao haina mashaka watalipa tu. Lakini haki yao ya kusafiri kama abiria wengine bila tatizo hilo ndilo jambo linalotia huzuni na linahitaji kufanyiwa kazi. Maana tumezoea kuona wanafunzi wakiachwa vituo vya mabasi kwa makusudi.
Wanafunzi wanasukumwa nje ya mabasi kwa makusudi. Wanafunzi wakataliwa kuingia ndani ya basi kwa nguvu na matusi mabaya. Vita kila kukicha kati ya makondakta na wanafunzi. Hiyo ndio hali halisi ya wanafunzi.
Je tumeongeza nauli adha kama hizi zitakwisha?
Magic Thinker