Adha hii kwa wanafunzi hadi lini?

Adha hii kwa wanafunzi hadi lini?

Millionea

Member
Joined
Oct 9, 2012
Posts
58
Reaction score
18
Maswali ninayojiuliza katika sakata hili la kuongezeka kwa nauli ni mengi. Na mengine ni mazalia ya machungu ya adha na taabu wanazopata wanafunzi kwenye daladala.

Hoja yangu ni Je haki za wanafunzi zitaheshimiwa nauli ikipanda? Huduma kwa wanafunzi itaboreshwa nauli ikipanda? Na lini tatizo la wanafunzi litakwisha kabisa? Nani anawajibu wa kusimamia usafiri huu?

Nadhani, wanafunzi kulipa Sh 200 kwao haina mashaka watalipa tu. Lakini haki yao ya kusafiri kama abiria wengine bila tatizo hilo ndilo jambo linalotia huzuni na linahitaji kufanyiwa kazi. Maana tumezoea kuona wanafunzi wakiachwa vituo vya mabasi kwa makusudi.

Wanafunzi wanasukumwa nje ya mabasi kwa makusudi. Wanafunzi wakataliwa kuingia ndani ya basi kwa nguvu na matusi mabaya. Vita kila kukicha kati ya makondakta na wanafunzi. Hiyo ndio hali halisi ya wanafunzi.

Je tumeongeza nauli adha kama hizi zitakwisha?

Magic Thinker
 
Bahati mbaya waliopandisha nauli hawakuzungumzia handling ya wanafunzi. Kwa hiyo makondakta wataendelea na utamaduni wao ule ule wa kuwanyanyasa wanafunzi. Tumefikia mahali pabaya sana humu nchini.
 
Wabongo kwa kulalama? Then no action. SHWAIN

unanikaribia kwa akili! Yani mimi nataka wa_Tz wateseke wapate akili maana hata bila formal research inaonesha 90 % ni mbulula.
 
Wa-Tz tujiulize swali dogo tu kwamba; Huyu kavaa uniform anafanya kazi na mshahara analipwa, lakini halipi nauli
na mwingine kavaa uniform hana kipato chochote lakini anatozwa nauli, Je ni logic gani inatumika hapo kama si kumwambia mzazi afunge mkanda.

Na kwa hili mi' naonelea tuandamane tu maana tulikofikishwa hata mungu hapendi!!
 
amini isamini watoto wanateseka sana mana wanayanyaswa na watu wenye umri sawa na wazaz wapo vituoni na kwenye madaladala cha ajabu wanajifanya hawaoni, nalishawahi kumtandika konda mmoja stesheni pale kamsukuma mtoto hadi akaanguka nilimpa makonde kisawasawa huwa sipendi upuuzi
 
kila mtu abebe msalaba wake. ulipozaa ulijua kuna shule na wajibu mwingine kwa mtoto wako. daladala ni biashara kama zilivyo zingine kwa wakubwa na wadogo. ukitaka mtoto wako asipewe shida na kondakta anza kwanza kumpenda mwanao. mpe nauli ya kutosha kulipa daladala. kama unashindwa kumtimizia mtoto unasubiri wenye biashara ya daladala wamtimiizie atanyanyaswa tu. kwa wale wanaolipa nauli kamili ya daladala hawapati adha ya kusukumwa. Jaribu kwenda Uganda hakuna nauli ya Dent wala mkubwa wote nauili moja na ni Level seat. Mpende Mwanao kabla hujalazimisha wengine kumpenda!
 
kila mtu abebe msalaba wake. Ulipozaa ulijua kuna shule na wajibu mwingine kwa mtoto wako. Daladala ni biashara kama zilivyo zingine kwa wakubwa na wadogo. Ukitaka mtoto wako asipewe shida na kondakta anza kwanza kumpenda mwanao. Mpe nauli ya kutosha kulipa daladala. Kama unashindwa kumtimizia mtoto unasubiri wenye biashara ya daladala wamtimiizie atanyanyaswa tu. Kwa wale wanaolipa nauli kamili ya daladala hawapati adha ya kusukumwa. Jaribu kwenda uganda hakuna nauli ya dent wala mkubwa wote nauili moja na ni level seat. Mpende mwanao kabla hujalazimisha wengine kumpenda!
nakuona mtoto wa manji mjukuu wa bakhresa!
 
amini isamini watoto wanateseka sana mana wanayanyaswa na watu wenye umri sawa na wazaz wapo vituoni na kwenye madaladala cha ajabu wanajifanya hawaoni, nalishawahi kumtandika konda mmoja stesheni pale kamsukuma mtoto hadi akaanguka nilimpa makonde kisawasawa huwa sipendi upuuzi

safi sana kwa kumuadabisha konda huyo hata mimi sipendi mwanafunzi anyanyaswe nikiona laazima konda huyo nimpe anachostahili
 
kila mtu abebe msalaba wake. ulipozaa ulijua kuna shule na wajibu mwingine kwa mtoto wako. daladala ni biashara kama zilivyo zingine kwa wakubwa na wadogo. ukitaka mtoto wako asipewe shida na kondakta anza kwanza kumpenda mwanao. mpe nauli ya kutosha kulipa daladala. kama unashindwa kumtimizia mtoto unasubiri wenye biashara ya daladala wamtimiizie atanyanyaswa tu. kwa wale wanaolipa nauli kamili ya daladala hawapati adha ya kusukumwa. Jaribu kwenda Uganda hakuna nauli ya Dent wala mkubwa wote nauili moja na ni Level seat. Mpende Mwanao kabla hujalazimisha wengine kumpenda!

Dah. kweli akili hazifanani na kila mtu anamawazo tofauti.
Mimi nishamuona mwanafunzi aninuliwa kwenye siti na konda na kasema atalipa nauli ya mtu mzima.
Nishamuona mwanafunzi anazuiwa kuingia kwenye gari na anasema atalipa nauli kamili.

wewe Huwajuwi makonda hata mwanao umpe nauli ya watu watatu atembee nayo ila kaa ukijuwa konda akiona yuniform tu anamzuwia anona kuwa kimavi hicho
 
Back
Top Bottom