A
Anonymous
Guest
Habari .
Nianze kwa kusikitika kwa ukatili unaoendelea kwa wakazi wa Makabe (Makabe secondary)wanaohudumiwa na ofisi ya DAWASA Makongo Juu.
Tuna mwezi sasa maji hatuna na wala hakuna sababu yoyote ya msingi inayotolewa nini chanzo cha tatizo hilo .
Tuliambiwa kutakuwa na siku mbili za kupata maji kila wiki Ila cha ajabu hakuna chochote na wakazi tunapata shida kutafuta maji huku wakiacha wauza maji kwenye magari kufaidika ili hali wateja wao wa dawasco tunapata shida .
Tumekuwa hatupati haki yetu ya kimsingi Kama wateja wao kuhudumiwa ipasavyo na kupoteza mapato ya serikali .
Inapelekea huduma za kijamii na kiuchumi kukosekana hasa kwa wamiliki wa nyumba za kupanga kukosa wateja kutokana na shida ya kununua maji huku nyumba zikiwa na mifumo ya dawasco.
Ni ukatili na unyama kukosa maji kwa mwezi mzima tumekubali mgao kwa wiki basi yatoke angalau siku 2 .
Na sio kuwasha lisaa ama kutowasha kabisa mitambo naomba wahusika na waziri atambue hujuma hizi.