Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Kutokana na kero ya usafiri katika jiji la Dar-es-Salaam kwa wanaotumia usafiri wa umma(daladala na yale mabasi ya mwendokasi),nashauri serikali ije na mkakati wa muda mfupi wa kuruhusu gari ndogo aina ya Noah zitumike kusafirisha abiri nyakati za asubuhi na jioni ili kuondoa adha ya watu kutaka kuuana wakigombania kupata japo nafasi ya kusimama ndani ya daladala kwa baadhi ya route zenye abiria wengi mida ya asubuhi na jioni ambapo watu hutoka majumbani na kuwahi makazini mida ya asubuhi na jioni kurudi majumbani wakitokea makazini na wengine wakitokea seheme wanazofanya shughuli za kuwaingizia kipato kama biashara,n.k.
Magari haya yanaweza kusajiliwa kubeba abiri kwa mida itayoonekana ni tatizo mfano kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa mbili asubuhi kwa mida ya asubuhi na kuanzia saa 12 jioni mpaka saa tatu usiku kwa mida ya jioni ili kupunguza adha ya watu kugombania daladala na kusimama kwa muda mrefu ndani ya magari haya ya kubebea abiria na pia kuwawezesha watu kuwahi makazini asubuhi na majumbani mida ya jioni badala ya kupoteza muda mwingi vituoni kusubiri usafiri.
Huu unaweza kuwa ni mpango wa muda mrefu huku mpango wa kumaliza tatizo hili ukiendelea na huu unaweza kuwa ni ku-introduce matumizi ya mabasi makubwa ya ghorofa kama ilivyo katika nchi za wenzetu kwa zile route ndefu na zenye abiria wengi mfano Makumbusho kwenda Bunju,n.k sambamba na kuondoa kabisa daladala zinazotumika sasa katika route hizi ndefu na kuzielekeza katika route zingine fupi fupi ndani ya jiji.
Tukitumia mabasi makubwa faida mojawapo ni kupunguza msongomano wa magari barabarani kwakuwa daladala hizi zitakuwa zimeondolewa katika njia hizi ndefu na ambazo ndio zenye msongamano mkubwa wa magari.
Na pia ikiwezekana mkakati mmojawapo wa kupunguza foleni uwe ni kuweka tozo maalumu kwa magari binafsi yanayoingia maeneo kama yale ya katikati ya Jiji na kwingineko na hii iwe ni baada ya kuingiza magari haya makubwa na hivyo kuondoa kero ya usafiri na kwa maana hiyo tutakuwa tumeondoa ulazima wa kila mtu kutumia gari lake binafsi kufika baadhi ya maeneo ambapo mabasi haya makubwa yatakuwa yanafika.
Ni ushauri tu wahusika maana hii kero haionekani kupungua hata baada ya serikali kuhamia Dodoma bali inaonekana kuongezeka na hivyo kuwa chanzo cha shida na mateso kwa watumiaji wa usafiri wa umma katika jiji hili,