Adhabu kali ziwekwe kwa wanaotapisha vyoo kipindi cha mvua

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
1686558330404.png

Kumekuwa na tabia ya wananchi wasiostaarabika kufungulia chemba za vyoo(Kutapisha Vyoo) kipindi cha mvua zinaponyesha.

Hii tabia ya kishenzi ipo hasa Dar es Salaam mitaa ambayo miundombinu ya gari la kunyonya majitaka ni mibovu kiasi kwamba hapafikiki kwa urahisi. Pia wengine wenye tabia hiyo ni wale wanaokwepa gharama za gari la kunyonya majitaka.

Hii hali ni hatari sana kwa afya za wakazi wanaozunguka maeneo hayo maana kunaweza kuibuka magonjwa ya mlipuko yanayoweza kuathiri afya zao.

Mvua zinazoendelea sasa hivi Dar es Salaam zimesababisha mitaa ya uswahili kunuka mavi. Ukipita mitaa ya Kawe kwa mtani wangu GENTAMYCINE imejaa maji machafu meusi yanayonuka mavi. Mbaya zaidi utakutana na vitoto vya shule vinapita kwenye hayo maji machafu bila hadhari.

Mitaa ya Sinza kimvua cha dakika 10 lakini baadhi ya mitaa haipitiki na inanuka hatari.

Mkurugenzi wa NEMC Dkt. Samuel Gwamaka alipata kuonya kuwa Serikali haitakuwa na msamaha na watu wanaotapisha vyoo wakati wa mvua, lakini naona mamlaka hiyo imeshindwa kudhibiti uchafuzi huu.

Nashauri mabwana afya, wenyeviti wa mitaa kwa kushirikiana na raia wema kama mimi tushirikiane kuwabaini wanaotapisha vyoo.

Sheria kali sana zichukuliwe dhidi yao kwa kuhatarisha afya za watu wema.
 
Mtani bhana....haya...! Nimecheka mno.
 
Back
Top Bottom