Adhabu kwa coastal union

Adhabu kwa coastal union

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
2,652
Reaction score
4,593
Napenda kuuliza ili nifahamu. Wale wachezaji wa Coastal Union waliomfanyia fujo mwamuzi katika mechi yao dhidi ya Azam, je, wameishaadhibiwa? Kama ndio, ni adhabu ipi?

Kuna baadhi ya wachezaji wa Coastal walimzonga refa dakika za mwisho kabla mpira haujaisha, na mmojawapo wa sub alimpiga refa kwa kiatu ila hakikumpata vizuri maan refa alikuwa anarudi kinyume nyume. Kingempata usoni vizuri angejeruhuiwa vibaya. Pia, wachezaji wa Coastal wa Sub, walikuwa wanarusha makopo uwanjani. Hakika wakionesha nidhamu mbaya sana.

Huwa nafuatilia habari hasa za kusoma ila sijaiona hiyo habari ya adhabu, sasa labda ilitangazwa kwenye redio au tv.




Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Duh....! Roho yako itaridhika tu utaposikia MTU Kaadhibiwa..!

Waja Sie ...achana na sisi,Wazito Sana!!
 
Adhabu ya kumpiga refa inafanana na adhabu ya kutokupeana mikono!!!!!
🚮🚮🚮
 
Adhabu ya kumpiga refa inafanana na adhabu ya kutokupeana mikono!!!!!
[emoji706][emoji706][emoji706]
Ukisikia maajabu ya dunia mojawapo ni hili la TFF na Coast Union. Fujo zote zile uwanjani pamoja na Mabadi kumrushia Kiatu usoni mwamuzi. Timu nzima ameadhibiwa Mabadi tu, tena Mechi 3 Sawa na Chama aliyeshindwa kushikana mikono.
 
Ingekuwa ni Yanga, muda huu ile kamati yao ya masaa 72 ingekuwa imeshatoa adhabu tayari. Ila kwa sababu ni timu ya rais wa shirikisho, lolote linaweza kutokea
 
Mbona adhabu tayari ilishatangazwa?
Tuwekee sasa ili tuione, na pia kujiridhisha iwapo inaendana na hayo makosa.

Lakini pia tufahamu kama huyo mwamuzi aliyesababisha hizo vurugu kutokea ana makosa, au la.
 
Back
Top Bottom