Adhabu kwa Simba

ungeanza na refa kwanza
wale waliovunja viti ni wahuni tu walikua wanatafuta sababu za kufanya fujo
Kosa la mtu mwingine halilalishi mwingine kufanya kosa.
Wote waadhibiwe
 
Kwahiyo kama goli lao limekataliwa na la wapinzani limekubaliwa ukivunja viti ndio linafutwa?kwanini wasisubiri mpira uishe then wakakata rufaa?sasa wewe uliocheza Mpira na unaoupenda mpira je kuvunja viti kimewasaidia nini?
 
Chanzo ni hao wanaoandaa ligi nawanao chezesha ligi yani makosa yanayo onekana vzuri kabisa mtu yupo nyuma kabisa anaona kosa lefa na wasaidizi wake hawaoni hatuwezi kulea upuuzi huo mpaka pale watakapo jirudi
 
Mleta uzi angekuwa na busara kama baadhi ya waleta uzi humu jf angeuliza kama waliofanya fujo ni vichaa au wana akili timamu, na kama siyo vichaa kwa nini fujo?? na siyo hukumu yenye lengo la kukata matawi badala ya kukata mizizi!!!
 
Kweli simba wahuni kabisa hawafai, waige ustaarabu wa Yanga kama walivyounesha mechi ya marudiano na TP Mazembe
 
mechi ya simba na yanga ni zaidi ya unavyofikiria yaani mtu kafunga kwa mkono iwe refalii kapitiwa au hajapitiwa siku nyingine usijekushangaa wakang'oa uwanja mfunge kwa mkono halafu watu wawachekee simba hawapendi ujinga
 
Mie simba
Lakini ujinga kama ule siungi Mkono kabisa
 
uwanja ule una security cameras! wanausalama wawabaini waliofanya vurugu mmoja baada ya mwingine tena kimya kimya. Baadaye watupe taarifa wakiwa tayari wameisha maliza kuwashughulikia.
 
Yaani viti 1700 vimeharibiwa,kila kiti kinathaman ya tsh laki mbili. Aisee hii hasara kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…