pantheraleo
JF-Expert Member
- Jan 5, 2013
- 692
- 880
Kocha zahera
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imempiga faini ya Sh 500,000 Zahera kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Ruvu Shooting iliyofanyika Agosti 28 mwaka huu kinyume cha Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo.
Kanuni hiyo ya 14(2m) inasema: “Kocha mkuu na viongozi wa benchi la ufundi wanawajibika kuvaa sare maalum za timu yao kwa benchi la ufundi.
Endapo kocha mkuu atahitaji kuvaa mavazi tofauti, anawajibika kuwa katika mavazi ya heshima na nadhifu. Ukiukwaji wowote utavutia adhabu kwa mhusika na / au kwa timu husika.” Mwisho wa nukuu.
Baada ya taarifa hizo za kocha Zahera kupigwa faini, mijadala mikubwa ikaibuka kwenye mitandao ya kijamii wengine wakisema ameonewa na wengine wakisema ni sahihi kwa Bodi ya Ligi kumpiga faini.
Mjadala mkubwa huko ni swaii ‘mavazi ya heshima na nadhifu ni yapi?’ Wengine wanamtetea Zahera kuwa hata kama anapenda kuvaa kaptula fupi na tisheti na chini bado yuko nadhifu na wengine wakisema ‘hapana hawi nadhifu’.
Chanzo:Mwananchi