Adhabu mavazi ya Zahera utata mtupu

Adhabu mavazi ya Zahera utata mtupu

pantheraleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
692
Reaction score
880

1567750464139.png

Kocha zahera

Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imempiga faini ya Sh 500,000 Zahera kwa kuvaa mavazi yasiyo nadhifu na ya heshima katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya Ruvu Shooting iliyofanyika Agosti 28 mwaka huu kinyume cha Kanuni ya 14(2m) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo.

Kanuni hiyo ya 14(2m) inasema: “Kocha mkuu na viongozi wa benchi la ufundi wanawajibika kuvaa sare maalum za timu yao kwa benchi la ufundi.

Endapo kocha mkuu atahitaji kuvaa mavazi tofauti, anawajibika kuwa katika mavazi ya heshima na nadhifu. Ukiukwaji wowote utavutia adhabu kwa mhusika na / au kwa timu husika.” Mwisho wa nukuu.

Baada ya taarifa hizo za kocha Zahera kupigwa faini, mijadala mikubwa ikaibuka kwenye mitandao ya kijamii wengine wakisema ameonewa na wengine wakisema ni sahihi kwa Bodi ya Ligi kumpiga faini.

Mjadala mkubwa huko ni swaii ‘mavazi ya heshima na nadhifu ni yapi?’ Wengine wanamtetea Zahera kuwa hata kama anapenda kuvaa kaptula fupi na tisheti na chini bado yuko nadhifu na wengine wakisema ‘hapana hawi nadhifu’.

Chanzo:Mwananchi
 
Wakati hiyo kanuni inapendekezwa mlikaa kimya hamkupeleka maoni yenu,TFF walivyoipitisha na kuitangaza mlikaa kimya.
Adhabu inatoka mnapiga kelele.
 
Siyo Africa, niletee kocha wa duniani huko aliyevaa kama zahera wakati wa mechi. Ukileta mmoja mimi nitaleta makocha 1000 na vaa yao.
 
Wamenuonea sana kaptura ni vazi la heshima Sana hasa kwa wanyasa wamalawi. Na sisi kaptra ni vazi la jeshi letu jwtz. Lipo alivaliwi siku hizi lakini lipo.
 
mi kila nikisikia Zahera mwinyi,nilijua ni binti fulani hivi wa kipemba,kumbe ni me?,hilo jina la mwanzo lilinichanganya
 
Wamenuonea sana kaptura ni vazi la heshima Sana hasa kwa wanyasa wamalawi. Na sisi kaptra ni vazi la jeshi letu jwtz. Lipo alivaliwi siku hizi lakini lipo.
Sometime tuache ushabiki ukiangalia vizuri vazi lake hilo sio bukta ni kinjunga Kuna tofauti Kati ya bukta na kinjunga.kinjunga sio vazi la heshima na tokea nianze kuangalia mpira sijawai kuona kocha kavaa kinjunga Bali nimeona wanao vaa bukta.
 
kwenye manvazi tff wamechemka hakuna sehemu yoyote ambayo hilo vazi limeonyesha utupu wake lakini hayo mavazi yalikuwa safi wala hayakuwa yamechafuka au kutopigwa pasi nachounga mkono ni adhabu aliyopewa kwa uropokaji wake
 
Hasira zao za litimu lao la ovyo ovyo kutupwa nje na vijana wa kimakonde wataka wazimalizie kwa Yanga! Pambaf kabisa
 
Huyu kazidi , hivi kaptura kama ni vazi la heshima kwanini watu wasivae kwenye mikutano?
 
Siyo Africa, niletee kocha wa duniani huko aliyevaa kama zahera wakati wa mechi. Ukileta mmoja mimi nitaleta makocha 1000 na vaa yao.
Siku ya Yanga na Ruvu shooting, kocha wa Yanga alivaa kaptula, wa Ruvu naye alivaa kaptula, sasa kwa nini adhabu ibague?
 
Tatizo hakutoa taarifa kama atavaa ngui tofauti na sare za klabu kama zilivyo kanuni
Pia yanga muwashukuru tff huyu zahera huwa anavaa hata jezi za kongo wakati wa majukumu ya yanga
 
Back
Top Bottom