Adhabu wanayostahili Simba ni kufungiwa kucheza bila mashabiki

Dadi Barnea

Member
Joined
Nov 30, 2024
Posts
40
Reaction score
33
Kwa uharibifu mkubwa uliofanywa na mashabiki wa Simba kung’oa viti vya Uwanja wa Benjamini Mkapa kipindi ambacho marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanywa na serikali katika Uwanja huo, adhabu pekee wanayostahili Klabu ya Simba ni kufungiwa kucheza bila mashabiki kwa kipindi cha mwaka mmoja, au hata zaidi.

Hiyo itakuwa ni njia sahihi ya kuwalazimisha mashabiki wa Simba kustaarabika; tunafahamu mashabiki hao wengi ni wakaazi wa Dar es Salaam mji ambao umekithiri kwa kuwa na raia wengi walio wavunjifu wa sheria, si barabarani ama hata maofisini.

Soma Pia:
Haitoshi tu kwa Klabu peke yake kulipia uharibifu huo, mashabiki lazima nao waadhibiwe.

Hiyo pamoja na rungu la CAF itatosha kuleta ustaarabu tunaoutarajia katika burudani na biashara ya mpira.
 
Kwa walichofanya lazima CAF iwafungie kuingiza mashabiki + faini kubwa
Waarabu nao watapigwa faini kubwa
 
Endeleeni kujidanganya caf sio tff caf awafati kelele za mitandaoni watafata taarifa ya kamishina wa mechi na polisi, na vile vile nawao wanawatu wao wa usalama
 
Ungesema tu wacheze bila mashabiki, hayo ya kufungiwa ungeyatoa maana unapoteza maana.
 
Kwa uharibifu mkubwa uliofanywa na mashabiki wa Simba kung’oa viti vya Uwanja wa Benjamini Mkapa kipindi ambacho marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanywa na serikali katika Uwanja huo, adhabu pekee wanayostahili Klabu ya Simba ni kufungiwa kucheza bila mashabiki kwa kipindi cha mwaka mmoja, au hata zaidi.

Hiyo itakuwa ni njia sahihi ya kuwalazimisha mashabiki wa Simba kustaarabika; tunafahamu mashabiki hao wengi ni wakaazi wa Dar es Salaam mji ambao umekithiri kwa kuwa na raia wengi walio wavunjifu wa sheria, si barabarani ama hata maofisini.

Haitoshi tu kwa Klabu peke yake kulipia uharibifu huo, mashabiki lazima nao waadhibiwe.

Hiyo pamoja na rungu la CAF itatosha kuleta ustaarabu tunaoutarajia katika burudani na biashara ya mpira.
Nyuma mwiko mnahangaika sana
 
Sababu za mashabiki wa simba kuvunja viti ni Nini?
Waarabu tunajua sababu wamefungwa.
Kuna wakati adui yako anafanya jambo ili uonekane mmbaya
 
Kwa uharibifu mkubwa uliofanywa na mashabiki wa Simba kung’oa viti vya Uwanja wa Benjamini Mkapa kipindi ambacho marekebisho mbalimbali yanaendelea kufanywa na serikali katika Uwanja huo, adhabu pekee wanayostahili Klabu ya Simba ni kufungiwa kucheza bila mashabiki kwa kipindi cha mwaka mmoja, au hata zaidi.

Hiyo itakuwa ni njia sahihi ya kuwalazimisha mashabiki wa Simba kustaarabika; tunafahamu mashabiki hao wengi ni wakaazi wa Dar es Salaam mji ambao umekithiri kwa kuwa na raia wengi walio wavunjifu wa sheria, si barabarani ama hata maofisini.

Haitoshi tu kwa Klabu peke yake kulipia uharibifu huo, mashabiki lazima nao waadhibiwe.

Hiyo pamoja na rungu la CAF itatosha kuleta ustaarabu tunaoutarajia katika burudani na biashara ya mpira.
Itakuwa ni kosa kubwa sana kuifungia Simba kwani waliosababisha hasara pale kiwanjani ni mashabiki wa Yanga waliovaa jezi za Simba.
 
MWAKA 1961 TANGANYIKA IKIPATA UHURU.

BABA WA TAIFA ALIWATAJA MAADUI WAKUU WA TATU WA TAIFA.
1. UMASIKINI.
2. UJINGA.
3. MARADHI.

AKAMALIZA KWA KUSEMA "MAADUI HAWA NI MAADUI KWELI KWELI NA SI MAADUI WA DHIHAKA"
JK NYERERE.
 
N

A hili limedhihirika kwa mashabiki wa simba
 
Kufungiwa kucheza bila mashabiki=kucheza na mashabiki wakiwepo uwanjani. Mleta mada hajui hata ameandika nn
 
Hii ni mara ya pili viti vimeng'olewa kwenye uwanja wa Taifa, halafu mashabiki ni wale wale!! Hivi shida ni nini?
 
Kufungiwa kucheza bila mashabiki ama kufungiwa kucheza na mashabiki? Kwenye logic ni kuwa sentensi negative umeinegate na kuifanya iwe true.
Sasa utafungiwaje kucheza "na"??? unafungiwa kucheza "without", siyo "with"....we vipi shehe
 
Mkuu unafungiwa kucheza na mashabiki siyo kufungiwa kucheza bila mashabiki
Kwenye logic -T=F na -F=T kwa hiyo -(-T)=F
 
Back
Top Bottom