Adhabu ya Bunge kwa Mpina inatoa taswira halisi jinsi gani Bunge na serikali ya Tanzania inavyowaona wananchi

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Bunge limtoa adhabu ya juu kabisa kwa kile kinachoonwa ni dharau ya Mpina kwa Spika wa Bunge. Na kwa kifupi sana, bila kutoa maelezo kamati ya maadili imetamka kwamba Bashe hakusema uongo, ikimaanisha kwamba ushahidi alioutoa Bashe, ambao uko wazi sana ni jinsi gani Bashe alidanganya, unaonwa kuwa ni uongo.

Mtu yeyeote mwenye akili timamu atajua ni nini kinachoendelea hapa, na wabungewote wenye akili timamu hawakutaka kumdadili Mpina, kwa kuwa wanajua nini kiko nyuma ya pazia juu ya suala hili la sukari - kulinda wale waliopo juu, ambao waliamua kutumia biashara ya sukari kujifaidisha wao na famiia zao. Kuna baadhi ya Wabunge hata walisema wao wanamwachia Mungu, kwa sababu anaona kila kitu wanachofanya. Kauli ya kumwachia Mungu jambo hili ilipotolewa wabunge wengi waliinamisha vichwa vyao chini kwa aibu na "remorse".

Kwa hiyo basi, hii inamaanisha nini kwa sisi wananchi ambao tunaliona hili kuwa Bunge letu? Kwanza kabisa, ni kwamba Bunge hili limetukana sisi wananchi, limeonyesha wazi haliko na wananchi, bali liko pale kutumikia watu fulani katika ubinafsi na ufisadi wao, katika hujuma yao dhidi ya nchi hii. Pili ni kwamba wananchi tumedharauliwa sana, na hata zaidi wale waliomchagua Mpina kama Mbunge wao. Bunge limeamua kwa makusudi kuwadharau, dharau mbaya kuliko ile Mpina anayosema aliifanya kwa Spika.

Na niwaambie wazi, Spika wa Bunge anatumika tu, na hata kuna tetesi kuwa amekubali kutumiwa kwa sababu ya ahadi anazopewa. Ni mtu wa kuhurumiwa sana. Alitumika wakati wa awamu iliyopita, na anatumika katika awamu hii.

Mwisho niseme wazi, Bunge na serikali wanapaswa kutambua kwamba haya mambo yana mwisho wake, na mwisho wanaotulazimisha wazalendo halisi wa nchi hii tuutafute, hautakuwa mzuri kwao. Hilo ni dhahiri kabisa.
 
Wananchi tungekuwa na umoja na mshikamano kwa hili la mpina ndilo tulitakiwa kuandamana mpka bungeni kupinga adhabu hiyo na kuishinikiza serikali kuchunguza tuhuma za wizara ya kilimo na wazari wake

Lakini kwakuwa hatuna umoja leo kila mtu ananung'unika kivyake kimoyomoyo

Kwa hali hii serikali itaendelea kufanya ujinga huu bila woga
 
Ushahidi sehemu yake ni Mahakamani

Pale wamemuhukumu kwa kudharau kiti cha Spika
John

Soma hapa

Mbunge wa Mtera, Livingstone Joseph Lusinde amesema kutokana na tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhusu kumtuhumu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kuwa alilidanganya Bunge kuhusu sakata la Uagizaji wa Sukari, anatakiwa kufungiwa kuhudhuria vikao 15 vya Bunge

Je kasimamishwa kww kudharau kiti cha spika au kwa tuhuma za kumtuhumu bashe?
 
Lusinde ni empty set

Tuhuma za Mpina ni za Kitakukuru na KiDCI Bunge lililosheheni Darasa la 7 hata English ya kwenyei tender documents hawawezi kutafsiri 🐼
 
Watanzania tunataka sukari kwa bei himilivu, hayo mengine hayatuhusu!!
 
Bunge limetawaliwa na maamuzi ya kijinga, haya maamuzi yameshaingia kwenye DNA zao sasa wameyazoea na kuwa tabia zao.

Hii tabia ya hovyo inaachwa ikue ndio maana sasa kuna wajinga wanaoshangilia adhabu aliyopewa Mpina kupitia kamati iliyoundwa.

Lile bunge la kina Msukuma kama una akili timamu huwezi kulitumia ku prove anything wrong kwenye hii nchi, unless nawe uwe mjinga usiyejua vipimo so that utumie ujinga wa wenzio kuthibitisha your point.
 
Wameamsha mafuvu kufanya kazi
 
 
Bunge la CCM bado liko kwenye Mfuko wa Muhimili mwingine (Serikali)!
Kwa hiyo kazi yake ni kuitetea serikali kwa nguvu zote bila kujali imekosea au haikosea.
Hoja za Mpina zilikuwa zinagusa mpaka Ikulu,kwa hiyo Bunge lisingekuwa tayari kuona serikali inavuliwa nguo mbele ya wananchi.
 
Aiseeee aibu sana kma wabunge wanaongea na kutetea ufisadi
Kama isingekuwa ni namna Uchaguzi wa 2020 ulivyofanyika, ningesema hawa wabunge wamechaguliwa na wananchi wenyewe. Nasubiri kuona uchaguzi wa 2025 ili nikate shauri pia kwamba watanzania ni watu wa aina gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…