Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,194
Reaction score
1,365
"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong?"

Je, ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?

Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?

Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?

I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha. Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda?

What do you think?

 
yap ni sawa kuwa na hukumu ya kifo....
(kwa watu kama mafataki na wabakaji)

(ingawa kwa upande wa Dini especially Christianity hairuhusiwi
kumuhukumu mtu)
 
hii hukumu hata mimi nafikiri ni rahisi sana,ukizingatia mtu ana rest in peace bila taabu
Wanasema huwezi kujua machungu ya kifo hadi siku ya zamu yako!
Kimsingi Nia ya adhabu ya kifo ni partly kumwadhibu anayekuwa ametenda kosa, lakini pia ni kutoa funzo kwa wanaobaki, wajue kuwa kosa fulani lina implication fulani, and let me tell you broda, it works out!
 
Hukumu ya kifo ni upande mmoja na kutekeleza hukumu ya kifo ni upande mwingine. Suala la 'uhalali' wa hukumu ya kifo ni tete sana. Inategemea unatilitizama kutoka upande gani (na pande zipo nyingi!). Kwa vyovyote vile, mimi naamini uwepo wake unapunguza kwa kiasi kikubwa 'hamu' ya binaadamu mmoja kutaka kumuuua mwingine (kinyume cha sheria).
 
yap ni sawa kuwa na hukumu ya kifo....
(kwa watu kama mafataki na wabakaji)

(ingawa kwa upande wa Dini especially Christianity hairuhusiwi
kumuhukumu mtu)

Siongelei dini kabisa hapa ninaongelea manufaa yake au kufanya kwake kazi.. Je issue ya mafataki na wabakaji je sio adhabu kali zaidi kuwa-castrate ?; sababu kuwaua ni kuwapa - rest in peace na sidhani kama ita-act kama hindrance kwa crime kuwaua
 

Je kifungo cha maisha sio adhabu tosha (yaani kazi ngumu kila siku) haifanyi watu waogope kufanya hilo kosa ?, sababu hukumu ya kifo sidhani kama ni justice done kwa ndugu wa mfiwa tena wengine might argue ni adhabu ndogo kuliko jamaa angebaki maisha yake yaliyobaki anafanya kazi ngumu kila siku na faida ya hiyo kazi ngumu (kama anazalisha) iende kwa wale waliozurika..
 

Kaka nafikiri kifo sio adhabu,ni ngumu kusema kifo ni kibaya wakati hakuna mtu aliyeenda na kurudi kutuambia jinsi kifo kilivyo kibaya,....inawezekana kabisa huko ni kuzuri kuliko hapo,..binadamu kwa asili tunapenda kuogopa vitu tusivyovijua na kupuuzia tunavyovifahamu,...nafikiri kuwe na dhabu ingine yenye machungu kuliko hiyo ya kifo.

Hebu fikiria,mtu anlawiti vitoto,anaua watu kwa sababu na imani za kipuuzi,............hapa ni lazma mtu ajutie kile alicho kifanya
 
Hii issue ni ngumu sana, mara nyingine huwa nakaa nafikiria naona kama adhabu ya kifo sio nzuri, kwa sababu mhusika anaponyongwa kimsingi waliodhurika na matendo yake hawapati chochote na yeye pengine anaweza asipate nafasi ya kujifunza na kujuta kwamba nilichokifanya hakikuwa sawa, lakini mara nyingine unafikiri unaona kuna watu akili zao ni mboovu na adhabu yao ni hiyo hamna kitu kingine, mfano majambazi wanaovamia na kuua labda familia nzima watu kama hao unadhani utawafanyaje?
 
Siongelei dini kabisa hapa ninaongelea manufaa yake au kufanya kwake kazi.. Je issue ya mafataki na wabakaji je sio adhabu kali zaidi kuwa-castrate ?; sababu kuwaua ni kuwapa - rest in peace na sidhani kama ita-act kama hindrance kwa crime kuwaua
Hukumu ya kifo si kwa ajili yao tubali kuwapa peace of mind waliokosewa.. Na tukiwafunga kifungo cha maisha watakuwa wanaTumia nguvu zetu ku ishi (tax)
 
Hukumu ya kifo si kwa ajili yao tubali kuwapa peace of mind waliokosewa.. Na tukiwafunga kifungo cha maisha watakuwa wanaTumia nguvu zetu ku ishi (tax)
Watatumia nguvu zetu kama watakuwa wanakataa na kulala tu, tunaweza tukawafanya productive kwa kufanya all those unwanted jobs ambazo watu wengine hawataki kuzifanya.., na kama issue ni kuwafanya wasi-abuse watoto je castration sio effective method?
 

Ukizingatia method huenda ikawa ni sumu au umeme yaani dakika chache tu mtu ushakufa..., ingekuwa kifo ni kibaya kuliko ku-face reality watu wangekuwa hawajiui (wala hitler asingejimaliza angesubiri aendelee ku-enjoy maisha)
 
Hukumu ya kifo si kwa ajili yao tubali kuwapa peace of mind waliokosewa.. Na tukiwafunga kifungo cha maisha watakuwa wanaTumia nguvu zetu ku ishi (tax)
Wafungwa si kula kulala (hasa kwa tanzania). Huko wanafanya kazi za kila aina, kilimo, ujenzi, uhunzi nk.Na mazao wanayozalisha huwa yanauzwa na nadhani chakula pia wantumia kujilisha kwa kiasi kikubwa. Magereza hutumika kama vyuo vya mafunzo vile....wanafunzwa kazi mbali mbali kwa hiyo shaka ya kodi ondoa.Mi nadhani mkosaji anayestahili adhabu ya kifo ni heri tu apewe adhabu nyingine kali mpaka ajutie kosa lake. Hata waathirika wa kosa lake labda kwa njia hiyo watapata ahueni.
 
Kwa upande wangu kwa kweli sikubaliani na hukumu ya kifo na sidhani kama inaleta nidhamu kwenye jamii, kwamba wengine wataogopa kufanya mauaji!

Mabadiliko ya mtu hayatokani na hofu, bali inahitajika badiliko la ndani kujua kuwa kuua ni vibaya, na sipaswi kufanywa hivyo!
 
Kweli kabisa hata wale watu wanaofanya maovu sidhani kama huwa wafanya huku wanategemea kushikwa, pili kunaweza kukawa na adhabu ambazo ni ngumu na mbaya na zikawanufaisha hata wale waliotendwa mfano hata kama mkosaji ana mali nyingi kuweza kuwapa fidia waliokosewa as well as kufungwa na kufanya kazi ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…