Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

Adhabu ya kunyonga hadi kufa imepitwa na wakati?

Nafikiri ni bora hukumu ya kifo ipigwe marufuku. Justice is fallible. Imeshawahi kutokea watu wasio na hatia kupelekwa gerezani, ila kwa bahati nzuri bado tulikuwa na uwezo wa kuwaacha huru tena baada ya kugundua kwamba tulikosea. .

Mkuu hii ilishatokea mtu alinyongwa kumbe alikuwa hana hatia (na kwa hili kosa watu wenye ma-lawyer wazuri, serikali inaweza ikalipa fidia kwa kodi zetu mpaka ikashangaa..!!)

Colin Campbell Eadie Ross (11 October 1892 - 24 April 1922) was an Australian wine-bar owner executed for the rape and murder of a child which became known as The Gun Alley Murder, despite there being evidence that he was innocent. Following his execution, efforts were made to clear his name, and in the 1990s old evidence was re-examined with modernforensic techniques which supported the view that Ross was innocent. In 2006 an appeal for mercy was made to Victoria's Chief Justice and on 27 May 2008, the Victorian government pardoned Ross in what is believed to be an Australian legal first.[SUP][1]
[/SUP]
Colin Campbell Ross - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Adhabu Ya Kunyonga Hadi Kufa Kuangaliwa Upya

3174454.jpg


JajiMkuu wa Tanzania, Othman Chande amesema suala la adhabu ya kifo bado linashughulikiwa katika Tume ya Kurekebisha Sheria ili kuona kama kuna haja ya kuifuta ama kuendelea nayo.

Jaji Chande aliyasema hayo jana wakati wa maadhimisho ya miaka 16 ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) yaliyoambatana na uzinduzi wa jengo la kituo hicho. Alisema baada ya uchunguzi huo tume itaandika ripoti na kuikabidhi Serikali ambayo itaamua na kisha kulifikisha suala hilo bungeni.

“Adhabu ya kifo ni kitu ambacho kinamuathiri binadamu na itabidi nchi iamue kuhusu adhabu hiyo,” alisema Jaji Chande. Alisema kila mwaka nchi mbili hadi tatu zinafuta adhabu hiyo na kwamba msimamo wa Umoja wa Mataifa unataka nchi zote ziondoe adhabu ya kifo.

Hata hivyo alisema licha ya kuendelea kuwapo kwa adhabu hiyo nchini bado utekelezaji wake haufanyiki kwani ni muda mrefu watu waliohukumiwa kunyongwa hawajanyongwa.

Katika hatua nyingine, Jaji Mkuu ameitaka Serikali iandae na kukamilisha Sera ya Taifa ya msaada wa sheria ili Bunge litunge sheria itakayowasaidia watu wasiokuwa na uwezo wa kifedha wa kulipa mawakili.

Alisema watu wengi wamekuwa wakikosa haki zao kutokana na kukosa msaada wa kisheria na kwamba hata mawakili walioko ni wachache ukilinganisha na idadi ya Watanzania wote ambao ni zaidi ya 40 milioni.

Alisema Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa katika utoaji haki nchini zikiwamo urithi wa kimila unaowafanya wanawake wengi kunyimwa haki ya kurithi mali walizochuma na waume zao.

Chanzo: Mwananchi
 
Those who kill innocent people (intentionally) must be killed..
 
Hili suala la uhalali wa adhabu ya kifo ni moja kati ya masuala magumu sana katika falisafa ya ujinai na utoaji wa adhabu kama lilivyo gumu katika falsafa ya sheria na haki. Tukilitizama kwa haraka haraka tunaweza kusema kama ni kuondoa kosa kwa kosa. Wengine watasema ni kuondoa moto kwa moto kama ilivyo dawa ya moto ni moto. Wengine watasema ni negation of negation kwamba negative plus negative unapata postive ili mradi falsafa nyingi zinatumika kuhalalisha au kuhalamisha adhabu ya kifo.

Adhabu ya kifo una uhai mrefu kama ulivyo uhai wa binaadamu. Katika maandiko matakatifu karibu ya dini zote Mungu anasema aliyeuwa anastahili adhabu ya kifo. Waliosoma vizuri Biblia na Quraan watanisaidia. Katika dini zetu za asili akina "Murungu wa Kasanga" nakadhalika nao wamenukuliwa kufundisha hivyo. Tulipoingia katika curcularizarion bado adhabu ya kifo iliendelea kutumika katika makosa makubwa hata bada ya falsafa ya haki za binaadamu, ikiwemo haki ya kuishi kuingia katika sheria za mataifa mbalimbali ya dunia. Hoja ambazo zimekuwa zikitolewa juu ya uhalali wa adhabu ya kifo katika mtizamo wa haki za binaadamu ni kwamba adhabu ya kifo inakuja kama "necessity" ili kulinda mslahi ya wengi. Katika Katiba yetu, kama zilivyo Katiba za nchi nyingi duniani ni kwamba adhabu ya kifo inahalalishwa katika maslahi ya umma pamoja na mambo mengine katika kutekeleza hukumu ya mahakama katika makosa makubwa kama uuwaji wa makusudi.


Kuulewa kama adhabu ya kifo ni mhimu au la kuna mambo kadhaa tunapaswa kuyajadili. La kwanza kabisa ni falsafa ya adhabu. Tunapotoa adhabu lengo letu linakuwa nini? Nijuavyo mimi adhabu inalenga katika mambo makuu matatu. Kwanza, kumrekebisha mkosaji. Pili, kuirekebisha jamii kwa kuifanya adhabu kwa mkosaji kuwa tishio na zuio kwao kufanya makosa kama hayo au zaidi ya hayo. Tatu kulipiza kisasi.

Kwa hali yoyote adhabu ya kifo haikusudii kumrekebisha mkosaji bali inakusudia zaidi kuwarekebisha wengine. Falsafa hapa ni kwamba mtu mmmoja aliyekosa anauwawa ili kuwazuia watu wengi zaidi wasiuwe watu wengine. Lakini pia adhabu hii ina sura ya kisasi. Kwamba, mtu aliyeuwa kwa makusudi anauwawa ili kuwafanya ndugu na jamaa zake na wote wasiopendezwa na hilo kuridhika na hivyo kutolipiza kisasi kwa kumuuwa mhusika na ndugu zake. Ukweli wa hili tunauona kila siku. Jamii ikimkuta mtu anauwa mtu mwingine kwa makusudi jibu la kwanza ni kumuuwa naye. Hayo yanaweza kuwa ndiyo maumbile ya wanaadamu. Ndivyo wanaadamu tulivyo. Au unaweza kusema ndivyo waafrika tulivyo (maana sijua ulaya na asia ni tofauti). Sheria kama zao la jamii haipaswi kupishana sana na jamii inavyoishi na inavyoaamini. Kwa hiyo basi, kama adhabu ya kifo bado inafaa Tanzania au la ni watanzania walio wengi tunapaswa kujibu na sio wanaharakati au serikali kukimbilia haraka haraka kubadili sheria. Athari yake inaweza kuwa kubwa sana.

Chukulia mfano wa mauwaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi. Yalipamba moto. Baadhi yao wakakamatwa na kupelekwa mahakamani na hatimaye kuhukumiwa adhabu za kifo. Hivi sasa matukio yamepungua sana. Kwa nini? Watu wanajua wakiuwa ndugu zao makusudi nao watauwawa. Ni wwangapi waliokuwa na mawazo ya kuuwa ndugu zao wakazuiwa na kuogopa adhabu ya kifo bila shaka ni wengi. Kama hivyo ndio ndivyo kuna uhalali wa kuuwa mtu mmoja kwaajili ya kuokoa wengi.

Naomba niishie hapo niwapishe wenzangu kuchangia
 
Kuna mjumbe mmoja ametoa hoja nzito na ningeomba pia niichangie. Anazungumzia kuhusu matukio ambayo mtu anahukumiwa adhabu ya kifo na mbele ya safari anaonekana kuwa hakuwa na hatiya. Hilo ni moja ya maswali magumu katika uhalali wa adhabu ya kifo.

Mimi msimamo wangu juu ya hilo ni kwamba adhabu ya kifo zotolewe tu katika kesi ambazo mtuhumiwa amehukumiwa na kutiwa hatiyani kwa ushahidi wa moja kwa moja na sio ushahidi wa kimazingira. Pia mahakama ziwe na uhuru kulingana na mazingira yanayoizunguka kesi kutoa hukumu ya kifungo cha maisha badala ya adhabu ya kifo.

Sheria iweke wazi mambo ambayo jaji anapaswa kuyazingatia anapotoa adhabu ya kifungo cha maisha badala ya adhabu ya kifo na hiyo iwe katika execeptional curcumstances.
 
Ndugu yangu VoiceofReasons jibu la swali lako linaweza kuwa rahisi sana. Nenda leo gerezani kwa watu waliohukumiwa adhabu ya kifo. Muulize mmoja mmoja yupi angependa kunyongwa na yupi angependa kufungwa kifuko cha maisha.

Sina wasi wasi wowote kwamba zaidi ya asilimia tisini watapenda kufungwa kifungo cha maisha. Maisha matamu ndugu yangu na kifo kichungu. Gerezani japo watu hawana uhuru wanaishi. Wanakula, wanaongea, wanafurahi siku nyingine, wanafanya kazi, wanacheza na wanapambana na kifo wanapougua kama walivyo watu waliohuru
 
Kunamchangiaji mmoja anasema adhabu ya kifungo cha maisha ndio muafaka sana kwakuwa alieko gerezani hawezi kufanya kosa. Naomba kutofautiana naye kwa hilo, pamoja na mambo mengine. Kuna ushahidi mwingi wa kutosha nchini na nje ya nchi ya wafungwa wanayofanya makosa makubwa hata uuwaji ukiondoa makosa ya kawaida kama kuingiliana kinyume cha maumbilke, kupigana, nk.

Kuna wanaosisitiza adhabu ya kifungo cha maisha na kufanya kazi ngumu kwa kuwa ni productictive. Kiuchumi wanaweza kuwa sahihi. Lakini lengo la msingi la adhabu sio uzalishaji mali bali ni kuzuia makosa hasa kwa wanajamii. Pili, kufanya kazi japo ni adhabu ni sehemu mhimu ya maisha ya mwanaadamu. Kazi ndio inayomtofautisha mwanaadamu na wanyama.

Ndio maana katika maandiko tunaambiwa asiyefanya kazi asilie. Kwa hiyo kazi, kimsingi sio adhabu bali ni sehemu ya maisha na mahitaji ya kimaumbile ya mwanaadamu. Jitu kama limeweza kutoa roho ya mwenzake kwa ukatili kabisa litaoona adhabu kushika jembe tu na kulima kazi ambayo ni sehemu ya maisha yetu?
 
Ndugu yangu VoiceofReasons jibu la swali lako linaweza kuwa rahisi sana. Nenda leo gerezani kwa watu waliohukumiwa adhabu ya kifo. Muulize mmoja mmoja yupi angependa kunyongwa na yupi angependa kufungwa kifuko cha maisha. Sina wasi wasi wowote kwamba zaidi ya asilimia tisini watapenda kufungwa kifungo cha maisha. Maisha matamu ndugu yangu na kifo kichungu. Gerezani japo watu hawana uhuru wanaishi. Wanakula, wanaongea, wanafurahi siku nyingine, wanafanya kazi, wanacheza na wanapambana na kifo wanapougua kama walivyo watu waliohuru

Sasa ukiwauliza wahukumiwa unategemea jibu gani? Yaani unataka waulizwe adhabu gani watakuwa comfortable nayo?
 
Huo nimetowa kama mfano kuthibitisha kwamba wahalifu wengi na wasio wahalifu wanaogopa adhabu ya kifo kuliko kifungo cha maisha
 
"Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"​


Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?

Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?

I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha...Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda....

What do you think?.....

Mimi napinga adhabu ya kifo maana "it's the most inhumane punishment." Kama judge Mwalusanya alivyosema kwenye moja ya hukumu zake kuhusu adhabu ya kifo: "Serikali haiwezi kuwafundisha wananchi wake kutoaua kama yenyewe inawaua." Huwezi kufundisha mtu kuacha kutenda kitu kibaya kwa wewe kutenda hicho kitu kibaya bali utaweza kumfundisha tu kwa kuacha kutenda hicho kibaya. Baadhi ya watu wamekuwa wakisema "jino kw jino": je, mtu akilawiti mtoto na ili kuonesha kuwa kitendo alichokifanya ni kibaya naye atalawitiwa? Na je, huyo anayemlawiti "yule mlawiti" wa kwanza anakuwa hajalawiti?

Vivyo hivyo, kwa adhabu ya kifo. Kama mtu ameua afundishwe kwamba kuua ni vibaya na asaidiwe kurekebisha tabia na kuwa mtu mzuri tena. Ukiangalia mfumo wetu wa utoaji haki ulivyo kuanzia polisi hadi mahakamani ni wazi kwamba mtu "innocent" ni rahisi kuhukumiwa kifo na mtu "guilty" kuachiwa huru kutokana na kuendekeza rushwa na kubambikia kesi.

Halafu kuna baadhi ya nchi, ilishatokea wale waliopewa adhabu ya kifo kwa vile hawakunyongwa kwa mara moja, wahusika wenyewe walijitokeza na kukiri wao ndio walioua. Pili, kuna kesi hukumu zilibadilika baada ya kuwa ushahidi mwingine wa kumtoa mtuhumiwa wa mauaji kupatikana. Kutokana na mazingira kama haya, adhabu ya kifo haina maana tena. Imekaa zaidi kama kulipiza kisasi na siyo kumrekebisha mtuhumiwa/mfungwa.
 
Ndugu yangu VoiceofReasons jibu la swali lako linaweza kuwa rahisi sana. Nenda leo gerezani kwa watu waliohukumiwa adhabu ya kifo. Muulize mmoja mmoja yupi angependa kunyongwa na yupi angependa kufungwa kifuko cha maisha. Sina wasi wasi wowote kwamba zaidi ya asilimia tisini watapenda kufungwa kifungo cha maisha. Maisha matamu ndugu yangu na kifo kichungu. Gerezani japo watu hawana uhuru wanaishi. Wanakula, wanaongea, wanafurahi siku nyingine, wanafanya kazi, wanacheza na wanapambana na kifo wanapougua kama walivyo watu waliohuru

Kwahiyo mkuu issue ni kwamba tatizo adhabu sio kali sana watu gerezani ni kama wapo likizo na wanachokosa ni uhuru tu.., lakini kama wangepata adhabu kali tena wakafanya kazi ambazo zikasaidia jamii husika nadhani watu wangeomba Mungu wafe kuliko kupata hayo mateso.., kwahiyo badala ya kuua unaweza ukaongeza suffering kwa waliofungwa ili kuhakikisha wanajuta na ku-suffer
 
Mnapochangia mada hii kumbukeni mambo yafuatayo. 1) Kuna mtu amedhulumiwa haki yake ya kuishi na mtu ambaye bado ana-enjoy hewa saafi. 2) Wapo wakosaji wengine ambao wanatakiwa kufundishwa kuwa kuwa ni vibaya na ni dhambi hawa lugha wanayoelewa ni kuuliwa maana ndo mana na wao walitoa adhabu hiyo. 3) Tutakapo punguza adhabu ya wanaowauwa wenzao tunataraji nini kuongezeaka kwa makosa ya mauaji au kupunngua na 4)

Baada ya kuwasamehe wauwaji na kuwapunguzia adhabu wanaokabiliwa na makosa ya mauaji, wafiwa tuwafikirie kuwalipa maana hawatajisikia vema kujua kuwa waliowauwa ndugu zao bado wanatesa na huenda wakatoroka. Unapaswa kuangalia pia watu hawa wanaouwa ni watu wenye upungufu wa akili tunawaepuka namna gani tunapoishi nao mtaani bila vitambulisho maalum.

Adhabu ya kifo iendelee ili Malbino waishi kwa amani, Dada zetu wanaouliwa kwenye magest wapunzike na nasi tuwe na imani kuwa mara tutakapodhulumiwa uhai basi taifa litatulilia kwa kulipa kisasi.
 
Mnapochangia mada hii kumbukeni mambo yafuatayo. 1) Kuna mtu amedhulumiwa haki yake ya kuishi na mtu ambaye bado ana-enjoy hewa saafi.
Wengine watasema kwamba kuua ndio unampa adhabu ya haraka na ya kuisha haraka kuliko kubaki hai na kupewa mateso kila siku ya uhai wake uliobakia (yaani unampumzisha na shida ambazo angepata duniani)


2) Wapo wakosaji wengine ambao wanatakiwa kufundishwa kuwa kuwa ni vibaya na ni dhambi hawa lugha wanayoelewa ni kuuliwa maana ndo mana na wao walitoa adhabu hiyo.
3) Tutakapo punguza adhabu ya wanaowauwa wenzao tunataraji nini kuongezeaka kwa makosa ya mauaji au kupunngua na
Statistically inaonyesha kwamba hukumu ya kifo haipunguzi watu kuuana sababu mtu huwa afanyi kosa akitegemea kushikwa yeye anadhani hatashiwa ndio maana anafanya..,


4) Baada ya kuwasamehe wauwaji na kuwapunguzia adhabu wanaokabiliwa na makosa ya mauaji, wafiwa tuwafikirie kuwalipa maana hawatajisikia vema kujua kuwa waliowauwa ndugu zao bado wanatesa na huenda wakatoroka.
Hatusemi kupunguza adhabu lakini Je hakuna adhabu kali na ya kutesa kuliko kuua (sababu ni wangapi huwa wanajiua ili kukimbia matatizo ya dunia).., kwahiyo kuliko adhabu ya kuisha kwa haraka wanaweza wakapata mateso na kazi ngumu gerezani na kila pato wanaloingiza kama lipo kupewa victims wao

Unapaswa kuangalia pia watu hawa wanaouwa ni watu wenye upungufu wa akili tunawaepuka namna gani tunapoishi nao mtaani bila vitambulisho maalum. Adhabu ya kifo iendelee ili Malbino waishi kwa amani, Dada zetu wanaouliwa kwenye magest wapunzike na nasi tuwe na imani kuwa mara tutakapodhulumiwa uhai basi taifa litatulilia kwa kulipa kisasi.

Mkuu kisheria ukishaonyesha kwamba mtu hana akili (mens rhea) basi huyo hawezi kunyongwa sababu hata akiua inaoneka kwamba hakukusudia, na mpaka sasa hawa watu wasio na akili wanapelekwa kwenye medical care na sio gerezani, unless tuanzishe sheria ya kuua vichaa
 
Mnapochangia mada hii kumbukeni mambo yafuatayo. 1) Kuna mtu amedhulumiwa haki yake ya kuishi na mtu ambaye bado ana-enjoy hewa saafi. 2) Wapo wakosaji wengine ambao wanatakiwa kufundishwa kuwa kuwa ni vibaya na ni dhambi hawa lugha wanayoelewa ni kuuliwa maana ndo mana na wao walitoa adhabu hiyo. 3) Tutakapo punguza adhabu ya wanaowauwa wenzao tunataraji nini kuongezeaka kwa makosa ya mauaji au kupunngua na 4) Baada ya kuwasamehe wauwaji na kuwapunguzia adhabu wanaokabiliwa na makosa ya mauaji, wafiwa tuwafikirie kuwalipa maana hawatajisikia vema kujua kuwa waliowauwa ndugu zao bado wanatesa na huenda wakatoroka. Unapaswa kuangalia pia watu hawa wanaouwa ni watu wenye upungufu wa akili tunawaepuka namna gani tunapoishi nao mtaani bila vitambulisho maalum. Adhabu ya kifo iendelee ili Malbino waishi kwa amani, Dada zetu wanaouliwa kwenye magest wapunzike na nasi tuwe na imani kuwa mara tutakapodhulumiwa uhai basi taifa litatulilia kwa kulipa kisasi.

Mwaka 2003 nilirudi Tanzania baada ya kuwa niko nje ya Tanzania tangu 1992. Nilikuwa na rafiki yangu kumtembelea mmoja wa "senior police officers", ambaye kwa muda huo alikuwa amestaafu. Rafiki yangu alikuwa padre wa Kanisa Katoliki na yule "senior police officer" alikuwa Mkatoliki pia. Kulingana na kazi aliyokuwa akiifanya, alidai alishaua watu 17 kwa pistol. Alidai kuwa "kila aliposikia mtumiwa wa ujambazi" yeye alijua moja la kutoa cha moto na kuondoa uhai wa hao watuhumiwa bila hata kujua sababu nyingine. Aliendelea kusema sasa amestaafu ila hana amani rohoni na anajaribu kusali rosali, kuvaa medalia na skapulari lakini wapi. Akamwuliza yule Fr: "Hivi hata mimi Mungu atanisamehe nitakapokufa?"

Nilivyosikia hivyo, nilimwonea huruma mzee wa watu (sijui kama alisha kufa au bado yu hai) na pia familia za wale waliouliwa kwa kutuhumiwa tu bila hata kuthibitisha kama wameua. Nimesema haya nikitaka kujenga hoja kuwa hata wanaofanya kazi ya kutekeleza hukumu ya kifo ukiongea nao watakueleza kuwa maisha yao siyo sawa kwa kukubali kutoa uhai wa mtu. Hii inaonesha tu kuwa hukumu ya kifo ni mbaya na hata kama mtu mmoja ameua haifai kurudiwa kwa mtu mwingine. "It's awful to kill or work as an executor/a state killer."
 
Kwamba adhabu na kazi wanazopewa Gerezani ni ndogo mimi naona sio kweli. Hoja yangu ilikuwa kufanya kazi kama kufanya kazi bila kujali ugumu wa kazi asili yake sio adhabu bali ni sehemu ya maisha ya mwanaadamu. Ndio maana huwa inaendana na kunyimwa uhuru kwa kufungwa.

Nijuavyo mimi kufungwa na kukaa ndani tu kuanzia asubuhi hadi jioni bila kufanya kazi ni adhabu kali kuliko kufungwa na ukapata muda mkubwa wa kufanya kazi. Chunguza. Nilichotaka kuonesha hapa ni kwamba hakuna adhabu inayoogofya kwa mtu mwenye akili timamu ya kawaida kama adhabu ya kifo. Maana, binaadamu wa kawaida mwenye akili timamu anapenda kuishi kuliko kitu kingine. Hawa wanaojiiuwa wengi kati yao wanafanya hivyo wakiwa katika matatizo ya kiakili au kisaikologia yanaweza kusababishwa na ugonjwa au msongo wa mawao kupita kiasi.

Ukimbaka aliyebakwa au kumuuibia aliyeibiwa kuna mafundisho gani kwa aliyeibiwa na jamii iliyo baki? Kwanza kubakwa anatendwa mwanamke na anaetenda ni mwanaume. Kisheria mwanaume hawezi kubakwa. Kama aliyeiba naye ataibiwa hiyo itakuwa ni biashara au marejesheano na sio adhabu. Maana nikikuibia shilingi laki moja nawewe ukaniibia unaweza kunikuta na laki moja hiyo hiyo au kama nimetumia 10,000 utanikuta na 90,000. Na hiyo ni mpaka unikamate. Sasa mimi nitaona tabu gani kurisk kuibiwa hela nilioibiwa kwa kuiba na nikijua kuna uwezekano wa kutokamatwa na hata nikikamatwa wataniibia tu fedha iliyobaki. Kwa mtindo huo wa adhabu si makosa yatakuwa ya kawaida.

Tuelewe kwamba adhabu zinatokana na namna tunavyoishi na ukweli wa maumbile yetu si vinginevyo. Ndio maana Biblia na Quraani kama vilivyo vitabu vya dini nyingine kama Budha na Hindu zinatamka adhabu hiyo japo inawezekana zilianza kwa nyakati tofauti. Hivyo hivyo dini zetu za asili hapa Afrika na sehemu nyingine za dunia. Watu hawa walikutana wapi na kukubaliana kwamba adhabu ya muuwaji ni kuuwawa?
 
Kwamba adhabu na kazi wanazopewa Gerezani ni ndogo mimi naona sio kweli. Hoja yangu ilikuwa kufanya kazi kama kufanya kazi bila kujali ugumu wa kazi asili yake sio adhabu bali ni sehemu ya maisha ya mwanaadamu. Ndio maana huwa inaendana na kunyimwa uhuru kwa kufungwa. Nijuavyo mimi kufungwa na kukaa ndani tu kuanzia asubuhi hadi jioni bila kufanya kazi ni adhabu kali kuliko kufungwa na ukapata muda mkubwa wa kufanya kazi. Chunguza. Nilichotaka kuonesha hapa ni kwamba hakuna adhabu inayoogofya kwa mtu mwenye akili timamu ya kawaida kama adhabu ya kifo. Maana, binaadamu wa kawaida mwenye akili timamu anapenda kuishi kuliko kitu kingine. Hawa wanaojiiuwa wengi kati yao wanafanya hivyo wakiwa katika matatizo ya kiakili au kisaikologia yanaweza kusababishwa na ugonjwa au msongo wa mawao kupita kiasi.

Ukimbaka aliyebakwa au kumuuibia aliyeibiwa kuna mafundisho gani kwa aliyeibiwa na jamii iliyo baki? Kwanza kubakwa anatendwa mwanamke na anaetenda ni mwanaume. Kisheria mwanaume hawezi kubakwa. Kama aliyeiba naye ataibiwa hiyo itakuwa ni biashara au marejesheano na sio adhabu. Maana nikikuibia shilingi laki moja nawewe ukaniibia unaweza kunikuta na laki moja hiyo hiyo au kama nimetumia 10,000 utanikuta na 90,000. Na hiyo ni mpaka unikamate. Sasa mimi nitaona tabu gani kurisk kuibiwa hela nilioibiwa kwa kuiba na nikijua kuna uwezekano wa kutokamatwa na hata nikikamatwa wataniibia tu fedha iliyobaki. Kwa mtindo huo wa adhabu si makosa yatakuwa ya kawaida.

Tuelewe kwamba adhabu zinatokana na namna tunavyoishi na ukweli wa maumbile yetu si vinginevyo. Ndio maana Biblia na Quraani kama vilivyo vitabu vya dini nyingine kama Budha na Hindu zinatamka adhabu hiyo japo inawezekana zilianza kwa nyakati tofauti. Hivyo hivyo dini zetu za asili hapa Afrika na sehemu nyingine za dunia. Watu hawa walikutana wapi na kukubaliana kwamba adhabu ya muuwaji ni kuuwawa?

Mkuu kwanza kabisa kifo ni kwamba kila mtu atakufa siku moja hakuna atakakimbia hii destination..; Pili kazi ngumu na mateso yanaweza yakawa makali kwa mtu hadi akatamani afe...; kuliko kuendelea kuishi (au hii haiwezekani) kwahio sisemi hawa watu wapewe kazi tu, bali kazi ngumu na faida ya hizo kazi kama ipo irejeshwe kwenye jamii husika.

Sisemi kabisa an eye for an eye..., sababu ukirejea maneno ya Gandhi anakwambia will make the all World go Blind..

Kuhusu dini kukubaliana na kwamba ukiua na wewe wakunyonge sidhani kama ni kweli labda sijarejea maandiko vizuri, nadhani maandiko mengi yanasema kusamehe au labda nikumbushe ni wapi maandiko yanasema mtu akiua na yeye anyongwe..
 
Back
Top Bottom