Matajiri na wanasiasa wanapeleka watoto wao shule bora ambazo hakuna mambo ya viboko. Watoto wa maskini ndiyo wanapigwa stiki na kuwa watu wazima waogawaoga.
Mkuu wewe unategemea mtoto anayesoma fedha schools,shule ambazo mzazi analipa 10+M mtoto asiwe na nidhamu? Ni muda upi mtoto atamisbehave? Karo yenyewe ni adhabu tosha kwa mzazi na mtoto,
Hebu niambie kwa shule zetu ambazo mtoto inabidi awahi shule asafishe mazingira na shughuli ndogo ndogo za shule azifanye, Leo hii umwambie no sticks hapo si hakuna kitu kitafanyika shuleni,kwanza mtoto mwenyewe asipomuona Mwalimu darasani anashangilia maana hana cha kupoteza,
Nimekuwa Mwalimu for years now lakini naamini mtoto Wa shule za kata hawezi kuwa na nidhamu au kuelekea pale anapoelekezwa bila viboko,nikiwa zamu Mara nyingi watoto wananiona Mimi mpole,zamu Yangu huwa najaribu kufuata haki za watoto eti kuchapa ni dhuruma dhidi ya mtoto na hakika sipendezwi na uchapaji mtoto lakini nakuambia siku Hiyo utakuta watoto wanafika shule saa mbili,unategemea usafi Wa mazingira wafanye walimu?
Ni ngumu mno ,hizo shule mnazosema kuwa hawachapwi watoto,kwanza mtoto hafanyi usafi Wa mazingira,kuna wafuaji Wa nguo zao,ni computerized schools ambapo Mara nyingi mtoto haandiki notes na pia karo zao ni kubwa,sasa ni muda upi Mwalimu atapata nafasi ya kutoa adhabu ?
Waambieni hao watetezi Wa watoto mashuleni huku hali ni ngumu,kuni za kupikia uji Wa shule zinaletwa na mtoto,usafi Wa mazingira unategemea mtoto,maji kwa ajili ya usafi vyooni yanaletwa na mtoto,sasa kama hakuna bakora unadhani haya yataletwa na nani?
Kwa sisi wakiristo tunaamini kuwa
Mithali 23:13
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.