Adhabu ya viboko shuleni bado ni halali katika nchi angalau 64. Tanzania inang'ara kwa kutozuia viboko

Nyani Ngabu na Kiranga kwa Marekani mfumo wa 'mateso' ya viboko kwa wanafunzi upo vipi? Ni 'adhabu' zipi hutolewa?

Sky Eclat na Rebeca 83 mfumo wa 'mateso' ya viboko kwa Uingereza upo vipi? Ni 'adhabu' gani hutolewa?
Marekani ni nchi yenye majimbo 50, hapo sijahesabu territories, na kila jimbo linaweza kuwa na wilaya (counties, boroughs, parishes) nyingi sana. Texas ina wilaya 254 nafikiri ndiyo inaongoza.

Na kila wilaya inaweza kuwa na "wilaya za kishule" tofauti.

Na kila state inaweza kuwa na sheria tofauti, na kila wilaya inaweza kuwa na sheria tofauti, na kila wilaya ya kishule inaweza kuwa na sheria tofauti.

Kwa hiyo hili ni jambo linalokwenda tofauti, angalau kwa jimbo.

Kwa habari zaidi, anzia kwenye wiki ya hili jambo hapa chini

 
Matajiri na wanasiasa wanapeleka watoto wao shule bora ambazo hakuna mambo ya viboko. Watoto wa maskini ndiyo wanapigwa stiki na kuwa watu wazima waogawaoga.
Mkuu wewe unategemea mtoto anayesoma fedha schools,shule ambazo mzazi analipa 10+M mtoto asiwe na nidhamu? Ni muda upi mtoto atamisbehave? Karo yenyewe ni adhabu tosha kwa mzazi na mtoto,

Hebu niambie kwa shule zetu ambazo mtoto inabidi awahi shule asafishe mazingira na shughuli ndogo ndogo za shule azifanye, Leo hii umwambie no sticks hapo si hakuna kitu kitafanyika shuleni,kwanza mtoto mwenyewe asipomuona Mwalimu darasani anashangilia maana hana cha kupoteza,

Nimekuwa Mwalimu for years now lakini naamini mtoto Wa shule za kata hawezi kuwa na nidhamu au kuelekea pale anapoelekezwa bila viboko,nikiwa zamu Mara nyingi watoto wananiona Mimi mpole,zamu Yangu huwa najaribu kufuata haki za watoto eti kuchapa ni dhuruma dhidi ya mtoto na hakika sipendezwi na uchapaji mtoto lakini nakuambia siku Hiyo utakuta watoto wanafika shule saa mbili,unategemea usafi Wa mazingira wafanye walimu?

Ni ngumu mno ,hizo shule mnazosema kuwa hawachapwi watoto,kwanza mtoto hafanyi usafi Wa mazingira,kuna wafuaji Wa nguo zao,ni computerized schools ambapo Mara nyingi mtoto haandiki notes na pia karo zao ni kubwa,sasa ni muda upi Mwalimu atapata nafasi ya kutoa adhabu ?

Waambieni hao watetezi Wa watoto mashuleni huku hali ni ngumu,kuni za kupikia uji Wa shule zinaletwa na mtoto,usafi Wa mazingira unategemea mtoto,maji kwa ajili ya usafi vyooni yanaletwa na mtoto,sasa kama hakuna bakora unadhani haya yataletwa na nani?


Kwa sisi wakiristo tunaamini kuwa

Mithali 23:13

Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
 
Adhabu sio fimbo tu,ziko adhabu zenye manufaa nyingi tu,kulima bustabi,kupiga deki,kusafisha mazingira ya shule nk
 
Mimi mwalimu naheshimu haki za binadamu sichapi mwanafunzi, simfokei , nafundisha kwa mujibu wa ratiba tu , natoa zoezi kwa mujibu wa miongozo ya wizara , asome asisome afanye mazoezi asifanye Mimi hainihusu , najali Sana salary na biashara zangu mtaani ,
 
Sitoi adhabu itamumiza mtoto wa mtu wala sipotezi muda kufuatilia nidhamu zao, najali salary nimetoka mbeya kuja dar kutafta hela wala sio kuchapa
 
Mtoto wa kitanzania anayesoma shule ya kata aliyekulia katikati ya nyumba za singeli au katika jamii iliyopinda huko Tarime uache kumchapa???

Unafikiri kwanini watoto wakienda jeshini wanakuwa na nidhamu sana na ukorofi na ujinga unaisha?

Watoto wachapwe lakini wasipigwe, kuna tofauti ya kuchapa na kupigwa.

Wakiume wachapwe matako, wakike wachapwe mikono lakini kwa idadi sahihi iliyoainishwa.

Hata Biblia inasema usimnyime mtoto viboko.

Muhimu ni usimpige Kofi, ngumi, mateke etc.
 
Nyie wazazi wa siku hizi ndio wapumbavu na kina junia wenu..

Mnaharibu watoto wala msisingizie walimu
 
Wewe ni mwalimu, umewahi kutana na mzazi anayekuja shuleni kuongea na walimu baada ya mtoto wake kuadhibiwa?

Watoto wetu tunawalea vibaya sana na wanakuwa watu wa ajabu sana, hakuna kitu wanaogopa zaidi ya kiboko. Na wasipoguswa mwalimu asiyechapa anadharaulika na hasikilizwi.
 
Baki na mwanao nyumbani, mawazo ya kijima ni bora kuliko kumlea mtoto wako kama yai na akaja kusumbua walimu shuleni, na hao watoto wenu ndiyo wanaharibu watoto wengine shule sababu watoto wana tabia ya kuiga wenzao.

Mimi ni mwalimu ,na nina exposure kuliko wewe, nimekaa shule miaka mitatu kujifunza jinsi ya kulea mwanafunzi kwa kila umri, Mtoto wa kiafrika anayelelewa kizungu ni janga zaidi kuliko mimi kuwa janga.

Leeni watoto wenu vizuri au baki nao muwafundishe nyumbani kwenu.
 
Na vice versa is true wapo walimu baadhi nao wapo wanaotumia fimbo ili wafanye ngono na watoto na wengine kumalizia hasira za matatizo yao ya ndoa nyumbani. Ukiona mwalimu anachapa sana lazma nyumbani ana matatizo, unakuta mwalimu ana matatizo ya ndoa au ya kiuchumi na hata ya kisaikolojia hasira anamalizia kwa watoto. Adhabu ya viboko ya viboko kwa watoto(below 18yrs) shuleni iendelee lakini iwe na udhibiti kama sheria inavyoolekeza siyo mwalimu kujiamulia idadi ya viboko la sivyo child abuse hususani sexual abuse itatumika hapo.
 
[emoji1787][emoji1787]mwalimu ukiwaza hivi kama wazazi wajinga na walioshindikana enzi zao wanavyowaza,utapata dhambi kwa Mungu na mtoto huyu baadae atakuja kukulaani sana kwanini ulimuachia akafanya anavyotaka.

jana ilizuka mada kijiweni,kuna mwalimu alikuwa anafanya kama wewe,hapigi mtoto wa mtu,ila akitoa kazi wanaofanya anawanakili sehemu,akarudia kama mara kadhaa akapata wanafunzi wake kadhaa wa kweli,waliobaki akawaamuru wawe wanatona nje akiingia.
mkuu wa shule nayeye akiwakuta nje anapita tu na kuwasalimia,baada ya kama mwezi hivi wakaanza kuulizana hatma yao[emoji23][emoji23].wakaona hapa tunapigwa fimbo kali kuliko fimbo zenyewe.
 
tuache sheria itadeal na watu wa namna hii.

muhimu jitahidi kumfanya mwanao kuwa na tabia malaya,mabayo itamwezesha kuishi na kila mtu.
hata mwalimu mwenye matatizo kwake hapigi mtoto mtiifu,si ndio!!!!!

unalea litoto kama yai,wataliua huko nje.wengine hawapendi ujinga.kama sio waalimu basi polisi.
 
Pole sana hata miye kuna mwalimu nna hasira naye hadi leo more than 20yrs..Serikali ilishatoa sheria na mwongozo zamanìiiii lakini haifuatwi mfano viboko mwisho ni vitatu na mwalimu wa kiume haruhusiwi kumchapa mwanafunzi wa kike, na kila adhabu ya viboko lazma mwalimu mkuu aidhinishe kwa maandishi nk nk lakini hakuna kinachofuatwa ni holela holela hadi walimu wachapaji wanatumia kama gia ya kubaka mabinti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…