Adhabu ya viboko shuleni bado ni halali katika nchi angalau 64. Tanzania inang'ara kwa kutozuia viboko

Wazazi wa akina junior hawataki hio , wanataka watt waende na school bus ,wale huko wakilishwa maharage wanahamishwa.

Wengine mnasoma shule kama mko Jkt [emoji23] unapigwa stick mpaka unajirekebisha kwa kila jambo.
 
Hufai hufai hufai mwalimu bomu wewe. Kwani kutomchapa mtoto ndiyo kumlea kama yai? Unaona sasa wewe umeshakariri kuwa mtoto asiyechapwa analelewa vibaya. Sikulaumu sana ila ndivyo unavyoamini na pengine ndivyo ulivyofunzwa. Mimi nimesoma education psychology hivyo najua ninachosema.

Nakuhurumia sana huko ulikosoma kuwa mtoto ni lazima achapwe siyo mafunzo hayo. Ninachosema hapa siyo kutoka kichwani mwangu ila ni research zimefanyika... tena nyingi na kugundua kuwa viboko vinaleta madhara kwa maisha ya baadae ya mtoto.

Ingekuwa viboko vinasaidia basi Afrika ambako shule nyingi zinachapa sana ingekuwa na wahitimu wenye faida kuliko nchi ambazo hawachapi.
 
Wewe mwenyewe bila viboko usingekua humu JF kuandika utopolo wako.
 
wazazi wa akina junior hawataki hio , wanataka watt waende na school bus ,wale huko wakilishwa maharage wanahamishwa..
wengine mnasoma shule kama mko Jkt [emoji23] unapigwa stick mpaka unajirekebisha kwa kila jambo
Kuna watu tunawakumbuka waalimu wetu kama dira,yaani unakiri kabisa mimi bila fulani sijui ningekuwaje.
 
Mimi sichapi kabisa. ,nichape niende jela nipotezee family yangu mwelekeo, Mimi nawaza tarehe ya salary 20-23 ya kila mwezi, aliyetayari kusoma atasoma asiye tayari poa tu nilitoka mbeya kuja hapa dar kutafta pesa sio kuchapa , walimu wenzangu punguzeni viboko ukichapa unambiwa una stress nk hapa nikupambana mtaani tu
 
Kuwa na kinyongo naye haisaidii nilitegemea useme unamshukuru,nikuulize kosa alilokuchapa nalo ulilirudia tena baada ya adhabu hii nzito?

Ukinijibu hapa nitajua kama alikuonea au hakukuonea.
Nimshukuru kwa lipi??
Inshort nlikuwa montress wa darasa hiyo siku sikuandika majina ya wafanya usafi nikamuachia moniter aandike tunatakiwa tuandike wote. Moniter akaenda kunisemea nikaitwa nlichezea viboko nlishindwa kula, na sikwenda shule wiki nzima sababu mikono nikama vile ilikuwa imekufa siwezi kushika chochote nalishwa chakula.

Yule teacher hiyo ndo ilikuwa tabia yake. Katesa Sana wanafunzi Sana shule adhabu Kali bila kosa la Maana na kufukuzisha wanafunzi shule Yani Kama vile alimroga Head master akisema hakutaki shule headmaster habishi unafukuzwa.

Mungu kamlaani saivi kawa Chapombe analala Bar machozi ya Watoto ya watu hajaenda bure.
 
,nikuulize kosa alilokuchapa nalo ulilirudia tena baada ya adhabu hii nzito?





Mimi nataka unijibu hilo swali hapo juu,baada ya kupewa hiyo adhabu nzito hadi kushindwa kula ilitokea tena ukaacha kufanya kazi yako kama ulivyoelekezwa?

Usishangilie mwenzako kuanguka kimaisha hayo wala siyo machozi ya watoto huyo no stress tu zinamsumbua mtu miaka sita hajaongezwa mshahara hata cent moja na maisha kioa siku yanapanda hilo ni kawaida!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…