ADILI CHAPAKAZI - PEKEE YANGU.

ADILI CHAPAKAZI - PEKEE YANGU.

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
ADILI HISABATI.
----------------------------------------

"Rapper mkongwe na hitmaker wa ngoma inaitwa ‘Peke Yangu’ Adili Mkwela a.k.a Hisabati .. nimefanikiwa kupiga nae stori nae kuhusu lifestyle yake kwa ujumla ndani na nje ya Sanaa.

Adili: in short jina langu naitwa " adili mkwela" a.k.a adili hisabati .

Katika hii sanaa nina kofia mbili kitu ambacho wengi hawajui mimi adili mkwela nje ya uimbaji mimi ni video producer ( video production" ) , nipo na kofia mbili..

1. Uimbaji
2. Video producer & director..

Tafsiri yake inatengemea jamii kwa ujumla inanitazama katika upande upi kwenye kazi zangu hizi mbili kwenye hii Tasnia ya Burudani nchini Tanzania..

Kuna watu wananifahamu kwenye upande wa ku - rap tu, " HIP HOP Raper" na wapo pia wanaotazama video za wasanii nilizotengeza mimi ila hawajui kuwa huo ni mkono wa adili hisabati..

Kwa mfano baadhi ya video nilizoproduce
Kwa producer & director..

1. Mwana F a - unanitega
2. Tmk wanaume family - ndio zetu
3. Marehemu mr ebo - kamango
4. Mh sugu - kiburi
5. Geez mabovu - nilipotoka mimi
6. Joh makini - hao
7. Nako 2 nako - kwaajili yako
8. Tmk wanaume halisi - ndege tunduni

Mdau ukiona logo ya chapakazi film ufahamu ni mimi adili chapakazi nimehusika mule kwa kiasi kikubwa kufinikisha shooting ya Project hiyo..

Ukwaju: nilikuwa nataka kufahamu ukweli kuhusu wimbo wako wa " pekee Yangu" je ilikuwa ni true stori ama ni wazo " idea " ya kufikirika tu .

Adili: pekea Yangu niliandika kiukweli ni true story.mimi nilikuwa na mwandikia msanii mike tee zamani, nyimbo zake nyingi sana almost 90% za nyimbo zake katika album yake nimeandimika mimi, which it's true.. jambo hilo hata mwenyewe Mike tee alikwisha wahi kulitamka kwenye " interview" zake kwenye vituo mbalimbali vya radio na Television ..

Kumuandimika msanii Mike tee Enzi hizo haikuwa big inshu & stori maana nilifanya muziki for passion, una msaidia tu mtu na wala utarajii kupewa chochote.

Tulisaidiana mimi na msanii Mike tee tukiwa kama marafiki wa karibu , kama ilivyo desturi marafiki wa kweli upeana support kwenye mambo mbalimbali wanayopitia kwenye maisha yao ya kila siku.

In short kwamba wasanii wote tunaishi kwa kutengemeana maana mimi ninaweza kuwa na uelewa wa jambo hili na mwezangu akawa na uelewa na kitu fulani kuhusu muziki zaidi yangu , vitu hivi viwili tukivikutanisha tunatengeneza kitu bora zaidi

Na mara zote jambo huwa likishirikisha mawazo ya watu wawili mara zote huwa ni bora zaidi, kuliko wazo ama mawazo ya mtu mmoja..

Huyu kabarikiwa hiki na wewe umebarikiwa kile mkiunganisha mnapata kitu kizuri, it's was easy coz wote Enzi hizo tulikuwa na passion ya Muziki, .

Kilichopelekea mimi kuandika wimbo huo kuna kipindi, Mike tee alipata project ya kufanya na producer P funk majani " katika studio za Bongo Records"...

kama sikosei nyimbo ilikuwa inaitwa " mnyalu" nyimbo aliyomshirikisha msanii " Ferooz",
Ile beat iliyotumika kurekodia huo wimbo mimi nilimuomba Rafiki yangu Mike tee anipatie ile Beat ili niweze kuitumia beat ile nyakati za Mazoezi yangu ya uimbaji na uandikaji wa mashairi / lycris, Maana mimi huwa ni mwandishi mzuri sana pale ambao nitakuwa naandika mashairi ya wimbo huku nikiwa nasikiliza mdundo wa Beat pembeni yangu, huwa kuna vibe fulani huwa napata kichwani changu tofauti kabisa nikiwa naandika mashairi bile beat.

Brain yangu ndio huwa inafanya kazi vizuri likija swala nzima la uandishi wa mashairi nikiwa na nasikiliza Beat huku naandika , kuliko kuandika mashairi bila Beat, huwa napitia wakati mgumu sana kuandika mashairi bila uwepo wa Beat pembeni yangu.

Niliipenda ile beat ikanipindi nimuombe msanii Mike ilinifanyie mazoezi..

Nilipomueleza Mike tee enzi hizo Mike tee anasoma pale kwenye Chuo cha C.B.E, akawa amieleza nifike pale Chuoni mida ya Saa nane mchana , ndio muda ambao yenue atakuwa free , akanieleza kwamba " kwahiyo Brother Adili ukifika pale chuoni utanishtua kisha mimi nitakupatia hiyo Beat .

Mimi kipindi hicho nilikuwa naishi Kijitonyama nikafanya maamuzi ya kwenda kwa mike tee nikachukua zangu usafiri hadi pale Chuoni C.B.E , nimefika pale nje ya geti la C.B.E namcheki Mike tee kwenye simu kisha mike tee anapokea simu kisha ananijibu " ety ooh nimeghahiri kukupa hiyo Beat Brother Am sory..

Kiukweli niliumia sana Moyoni mwangu nikakaa pale nje ya geti
Nikajiuliza muda wote tulipokuwa na mimi kuna inshu kibao mimi nilikuwa namsaidia , mara kadhaa nimemuandikia mashairi kwenye zile project zake za ghafla na zenye uharaka kufanyika hasa pale anapokuwa ameitwa na P funk majani " Bongo Records".. maana Enzi hizo msanii kupata chance kwa p funk majani kisha uichezee kwa nyakati zile ilikuwa ni kitu cha ajabu sana, maana kulikuwa na list kubwa sana ya wasanii wenye ahadi za kwenda kwa P funk majani kufanya kazi ( project & kurekodi).

Kwahiyo sometime majani alikuwa anamshtukiza msanii Mike tee nakumuhitaji studio , mimi nilikuwa natumia uwezo wangu wa kuandika Mashairi , namuandikia Mike tee haraka haraka kisha nampatia Mike tee na msanii mike tee enzi hizo alikuwa yupo fasta sana kukalili mashairi kwa hiyo kwake msanii mikee tee lilikuwa ni jambo rahisi sana kurekodi kazi / project kwa p funk majani kwa wakati sahihi bila kumiss ama misunderstanding na p funk majani sababu ya kuchelewa ama kukosea wakati wa kurekodi. Kama ilivyokuwa inatokea kwa baadhi ya wasanii kuchelewa kufika studio, ama makosa mbalimbali kujitokeza studio wakati wa kurekodi studio.

Mike tee katika hilo alikuwa msanii perfect sana, hakuhitaji wiki 1 ama 2 kukalili nyimbo mzee , ilikuwa almost kama two hours mtu tayari anakuwa amekwisha kalili everything.

Mfano kama nyimbo yake inaitwa " nampenda nani " aliomshirikisha msanii juma nature" hii ilikuwa ni project ya ghafla alinipingia simu nakunieleza jambo hilo na mimi sikuwa na hiyana fasta fasta nikamuandikia yale mashairi maana alinipitia Kijitonyama nyama nikaenda nae hadi mabibo almost kama dk 45 nikawa nimekwisha maliza kuandika mashairi ya wimbo huo unao itwa , " nampenda nani" ft. Juma nature.

Kisha mimi nikamuachia yale mashairi mimi kama kawaida yangu nikarudi zangu to my home street Kijitonyama ..

Vitu kama hivi viliniumiza sana mbona mimi kuna changamoto zake msanii mike tee nakuwa nipo fasta sana kumpa support ndani na nje ya Sanaa, mbona mimi changamoto zangu anakuwa hana time nazo.

Nikawa nimeunganisha na makosa ya watu wengine ninayokutana nayo katika jamii , kama unavyofahamu kasoro za wanadamu ndipo idea ya wimbo huo wa " pekee Yangu " ikipatikana .

Mimi adili chapakazi nilikuwa na zile lycris/ mashairi bile title ama jina la wimbo , ila Rafiki yangu wa karibu msanii wa Hip Hop marehemu Salu Tee, akanieleza mbona haya mashairi ni makali sana kama vipi mimi ninakupa title ama jina la wimbo " ndio wazo la marehemu Salu Tee nikalifanyia kazi na mashairi hayo nikayapa title ya " pekee yangu"..

By the time tunaenda kurekodi kwa p funk majani , producer majani lakini Base alipigwa producer ludigo , na vionjo vingine kama pale kwenye chorus ile sauti ya chini alikuwa producer bondea, ila mastering ni producer P funk majani na zile vocal aliingiza msanii Soggy doggy ..

Ila mandojo na domokaya mimi niliwafahamu kupitia "Bongo Records Tour " tulikuwa tumeenda kwenye tour Ya " Bongo Records" ilikuwa ni Tour ya wasanii waliosainiwa chini ya Record label ya Bongo Records huko mkoani Arusha" A town",

Tulikuwa hotel na mimi napiga stori na majani ghafla na wao wakafika pale hotelin kisha nao wakataka kuonana na Producer P funk majani , Enzi hizo bado hawajarekodi ngoma , nikapeana nao hi kisha marehemu mandojo akawa anacheza lile gitaa lake,

Nikaona kumbe wale jamaa ni wakali sana , ndio ikawa big story mule hotelini..
Producer P funk majani aliwaelewa sana wasanii hao mandojo & domokaya .

Hadi wanakuja Dar es Salaam kurekodi wimbo wao " nikupe nini" mimi Tayari nilikuwa nimekwisha wafahamu mandojo na domokaya na uwezo wao kwenye upande wa sanaa ya Muziki hapa Tanzania,

Ilikuwa ni jambo Rahisi kwa upande wangu coz mimi niliwafahamu tangu wakiwa Arusha wakiwa bado kufahamika ama kuwa watu maarufu Enzi hizo bado ni underground wanatafuta upenyo kwenye muziki huu wa Bongo fleva.

Ndio nikawafuata mandojo & domokaya nikawaomba wanifanyie tuning ya chorus kwenye ngoma yangu ya pekee yangu , mimi nilikuwa nimeandika kile kitu chorus hadi zile tuning yaani kwa kifupi nyimbo ilikuwa imekamilika nilichofanya mimi nikumpa tu maelezo marehemu mandojo & domokaya kwamba apite humu , nae mandojo & domokaya w akafanya kweli ngoma tukarekodi hadi leo ile ngoma ni moja kati ya track bora sana kufanyika hapa Bongo ,

ADILI HISABATI - PEKEE YANGU

Nimezaliwa pekee yangu na nitakufa pekee yangu/ siku ya hukumu ya mwisho itakuwa ni juu yangu/ sintakuwa na mtu ndani ya kaburi langu/ nitawaacha wote isipokuwa nafsi yangu/_Popote ninapokwenda lazima nijiamini/ hata kivuli changu hakita kuwa na mimi/ Dunia kama vita maadui pembeni yangu/ nina pingana kiume ama zao ama zangu/nimetoa upendo wa dhati kwa marafiki sadiki wengi wao ni wanafiki / Wana chuki fitina na ukatili/ zote zimeshamili kwenye imaya ya Adili/ shida zangu za kwangu/ na hata za kwao za kwangu/ hawana msaada kwangu bora nisote kivyangu / nilikwisha fadhili marafiki kadha wa kadha/ walipopata fedha walileta madaa/ nilichovuma kwao ni makovu na majeraha/Sintoshangaa maovu Dunia tabala mbovu wabaya ni marafiki wachache ni ndugu zangu/ thamani ya utu wangu najua haina malipo nadhani Mungu wangu anajua jinsi nilivyo/ Haki mbinguni Duniani ni dhulumati/ kamwe sidhani kuwa nanyi washigaji/Siwatamani Hahela na Dunia Bora pekee yangu

Pekee yangu - adili..🔥🔥

Vip kwa upande wako upo pamoja na ADILI..

Ama upo kivingine...

#funguka
Ukwaju wa kitambo

0767 542 202
 

Attachments

  • 1727338252505.jpg
    1727338252505.jpg
    230.5 KB · Views: 12
  • 1727338297269.jpg
    1727338297269.jpg
    187.2 KB · Views: 13
Sikuwa mpenzi wa bongohiphop ila hii ni kati ya ngoma kali sana. Flow, beat, lyrics, message. Inafaa kwa hali zote for cruising, deep reflection and meditation, workout session, vibing and jamming
 
Back
Top Bottom